Ads (728x90)

Mwandishi wa habari Ezekiel Kamanga akiinua pikipiki baada ya kugongwa na gari ambayo ilikatisha ghafla kushoto katika eneo la Mabatini leo saa 5 asubuhi wakati tukifuatilia tukio moja huko  Nzovwe.
Msamaria mwema akisadia kuinua pikipiki baada ya mimi kuruka kutoka kwenye hiyo pikipiki na kuanza kupiga picha za ajali hiyo, tulikuwa tukifuatilia tukio moja eneo la Nzovwe.
Gari hii ndiyo iliyotaka kubadilisha historia yetu leo hii asubuhi
Dereva wa gari lililotaka kubadilisha historia ya maisha yetu leo hii  mwenye tisheti ya Bluu bahari na jinzi akiomba msamaha kwa kosa alilolifanya kukatisha barabara ghafla na kutugonga.
Wasamaria wema hawakuchelewa kuja kutoa msaada eneo la tukio kila mmoja akitupa pole kwa tukio lililotusibu
Wasamaria wema wakiangalia ubovu wa pikipiki baada ya kugongwa na gari eneo la Mabatini leo asubuhi
Jamaa wakicheki ubovu wa pikipiki
Askari wa usalama barabarani naye hakuchelewa kufika eneo la tukio na kumuamuru dereva ageuze gari na kuliweka pembeni kwa maelezo zaidi.
Hii ndiyo gari iliyotugonga leo hii wakati tukielekea eneo la Nzovwe kufuatilia kero za kijamii.

Post a Comment