Kama ilivyo desturi ya wanataaluma ya Habari wanapokuatana bila kujali umri hakuacha kuchombeza maneno mawili matatu ya mas-hala ya kitaaluma na kuvunja mbavu kama anavyoonekana pichani akiwachekesha wanahabari.
MKURUGENZI
Mstaafu wa iliyokuwa Radio Tanzania RTD Bw. Abdul Ngarawa amesema kuwa weledi
wa kazi za uandishi wa habari umeporomoka kutokana na baadhi ya waandishi wa
habari kutotumia vipaji vyao na badala yake kuiga sauti za watangazaji
wengine kwa kukosea.
Bw. Ngarawa
amesema kuwa kazi ya uandishi na utangazaji mbali ya kuwa ni taaluma bali pia
inahitaji kipaji cha mtu binafsi na kwamba waandishi wanaopenda kuiga sauti za
watangazaji wa zamani wanakosea.
‘’Unapaswa
kutangaza wewe kama wewe ili watu wakukubali wewe kama wewe uwe na utambulisho
wako mwenyewe bila kuiga lahaja na sauti za wengine,’’anasema.
Alisema kuwa
watangazaji wa sasa wanapaswa kujitahidi kutangaza kulingana kutokana na
mazingira ya sasa kwa kujifunza zaidi na kufuatilia vyombo vingine vya habari
kwa kufuatilia sera na maadili yao kwa nia ya kuboresha taaluma na weledi
katika kazi ya Uandishi wa Habari na utangazaji.
Mzee
Ngarawa ameambatana na Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano
Nchini TCRA ambapo pamoja na na mambo mengine watatembelea vyombo
mbalimbali vya habari na Redio za FM zilizopo mkoani Mbeya ili kuibua na
kupata changamoto zilizomo katika Redio hizo.
|
Post a Comment