Ads (728x90)

Mkazi wa kijiji cha Chang'ombe, Kata ya Mkwajuni jimbo la Songwe Mbuke Kulwa akitafuta dhahabu katika mto mara baada ya kufukuzwa na mumewe ambaye alidai kuwa anaishi na mke mwingine,huu ni sehemu ya ukatili wa Kijinsia ambao Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA kimekuwa kikipinga na kukemea katika harakati zake za kupinga ukatili wa Kijinsia.

Kijana huyu Mwanafunzi wa shule ya Msingi Mkwajuni aliyejitambulisha kwa jina la  Asajile mkazi wa kitongoji cha Kamficheni Jimbo la Songwe Mkwajuni wilayani Chunya akitafuta dhahabu ili aweze kujikimu kutokana na mahitaji muhimu ya kila siku, Asajile ni miongoni mwa vijana wengi wa shule za Msingi ambao wamekuwa wakiacha masomo kwa na kwenda katika machimbo ya dhahabu wilayani Chunya.

Watoto hawa wakazi wa kitongoji cha Kigamboni kilichopo Jimbo la Songwe wilayani Chunya wakitafuta maji kwa ajili ya matumizi ya kila siku kutokana na uhaba wa maji katika mji huo,familia nyingi wilayani Chunya zimekuwa zikihangaika kusaka maji safi na salama kutokana na kukosekana mabomba ya maji kutosheleza kaya jimboni humo.

Mtoto huyu ambaye hakutambulika jina lake akiokota dhahabu ili kujipatia kipato kutokana na hali ngumu ya maisha yanayowakabili wakazi wa jimbo hilo.

Post a Comment