Ads (728x90)

Upandaji wa nyasi ukifanywa na watoto katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya


Watoto wakichukua nyasi kwa ajili ya kupanda katika uwanja wa Sokoine
Uwanja wa Sokoine unavyoonekana kwa sasa


Baadhi ya watu wakishirikiana na watoto kupanda nyasi katika uwanja wa Sokoine ambao wanadai kufanya kazi hiyo bila malipo

Watoto wakishiriki upandaji wa nyasi katika Dimba la Sokoine(Picha za watoto na Kennethy Ngelesi)
Hivi ndivyo Dimba la Sokoine linavyokuwa katika mechi mbalimbali za ligi, waau wahoji mapato ya uwanja huo yanaenda wapi.

Hivi ndivyo Dimba la Sokoine lilivyokuwa likionekana katika vyoo vyake.

Umati wa watu wanaohudhuria katika Dimba la Sokoine

Baadhi ya vitega uchumi vinavyouzunguka Uwanja wa Sokoine ambavyo wadau wanahoji mapato yake yanaenda wapi.


Picha za Uwanja Na Fasihi Media Inc.

IKIWA imepita miezi miwili tangu kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom na baadaye TFF kuamuru kufungiwa kwa uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya kutokana na kutokidhi vigezo,Wadau wa mchezo huo wamewatalekezea watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka 18 kuutengeneza uwanja huo.

Mwandishi wa habari hizi aliyetembelea uwanjani hapo alishuhudia kundi la watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 12 na 16 kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya wakipanda nyasi uwanjani bila malipo yoyote.

Baadhi ya watoto hao ambao walizungumza na waandishi wa habari walidai kuwa wanafanya kazi hiyo ya kupanda nyasi mchana kutwa lakini hakuna malipo yoyote ambapo pia wanadai kuwa wanashinda na njaa wakati wakitekeleza kazi hiyo.

Kutokana na hali hiyo  Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mbeya (MREFA) kimewaomba wadau wa mchezo huo mkoa wa Mbeya kujitolea kwa hali na mali kufanikisha zoezi la ukamilishaji wa uwanja huo ambao ni miongoni mwa viwanja Nane vilivyofungiwa kutokana na kutokokidhi viwango.

Mwenyekiti wa MREFA mkoa wa Mbeya Elias Mwanjala alisema kuwa tatizo la ukata la chama hicho limesababisha kuomba msaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka ili kuokoa jahazi na kwamba zoezi la upandaji wa nyasi katika uwanja huo linasuasua kutokana na kukosekana kwa fedha.
Hata hivyo Mwanjala alisema kuwa chama hicho kinaendelea kufanya juhudi kwa kushirikiana na timu zinazotumia uwanja huo za Mbeya City na Tanzania Prison kwa kuwaomba mashabiki wa timu hizo kujitokeza kusaidia kupanda nyasi katika uwanja huo.

Alisema kuwa tangu kuanza kwa utengenezaji wa uwanja huo wamepata msaada kutoka Jeshi la Magereza na Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao walijitolea gari kwa ajili ya kusomba nyasi na kuzifikisha uwanjani. 
Aidha Mwanjala alisema kuwa pamoja na mashabiki kujitokeza kupanda nyasi hizo chama chake kimekosa fedha za kuwasaidia angalau chakula wakati wakiendelea na kazi za upandaji wa nyasi hizo
Katika hali isiyo ya kawaida Mwanabloga Wetu alishuhudia makundi ya watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 12, 14 wakishiriki upandaji wa nyasi katika uwanja huo ambapo baadhi yao bila kujitaja majina walidai kuwa pamoja na kazi kubwa wanayoifanya kutwa nzima wanashinda na njaa na kwamba hawalipwi chochote.Mapema Blogu hii iliweka picha mbalimbali za Uwanja wa Sokoine kabla haujafungiwa ulioonesha baadhi ya vitega uchumi vya uwanja huo na umati wa mashabiki wanaoingia katika uwanja huo.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mbeya wamedai kuwa mara baada ya uwanja huo kukamilika uwekwe mkakati mbadala wa kudhibiti mapato yanayoingia wakati mchezo wa Ligi kuu kwa madai kuwa fedha zinazoingia hazilingani na hali ya uwanja huo.
''Mapato ya uwanja huo kuanzia sasa yadhibitiwe, inawezekana fedha zinazoingia zinapitia katika mifuko ya watu na hii ndio sababu umeona uwanja huu uko miaka mingi lakini mapato yake hayajulikani yalipo.
Meneja wa Uwanja huo Modestus Mwaruka hakuweza kupatikana kuelezea lolote juu ya mapato ya uwanja huo kutokana na simu yake kutopatikana kwa muda wote, hata hivyo jitihada za kumpata ili aelezee mustakabali wa uwanja huo ambao unamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea.

Post a Comment