Golikipa wa timu ya Simba Yaw Beko akichupa bila mafanikio baada ya mchezaji wa timu ya Mbeya City Deogratius Julius kufunga bao kwa njia ya Penati |
Wachezaji wa timu ya Simba na Mbeya City wakiwania mpira wakati wa mechi kati ya timu hizo uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, matokeo ya mchezo huo yalikuwa sare ya bao 1-1 |
Patashika wakati wa kuingia uwanjani |
Kocha wa timu ya Simba Zdravak Logurusic akifuatilia kwa makini mechi kati ya timu yake na Mbeya City leo jioni |
Kikosi cha Timu ya Mbeya City kabla ya mechi kati yake na Simba |
Kikosi cha timu ya Simba kabla ya mchezo kati ya timu yake na Mbeya City leo jioni yimu hizo zimetoka sare ya Bao 1-1. |
Magolikipa wa timu ya Simba Ivo Mapunda na Yaw Beko kabla ya mechi kati ya timu yao na Mbeya City timu hizo zilitoka sare ya Bao 1-1 |
TIMU za Mbeya City ya
Jijini Mbeya na Simba ya Dar es salaam zimelazimishana kutoka sare ya
Bao 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu iliyofanyika katika uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine leo jioni.
Uwanja
wa Sokoine ambao ulifurika wapenzi wa mpira walioanza kuingia uwanjani
saa 4.00 asubuhi ulishuhudia wapenzi na mashabiki wa kandanda wakitoka
uwanjani bila kutambiana baada ya timu zote kutoka sare ya bao 1-1.
Ilikuwa
ni Mbeya City ndiyo ilianza kuona lango la Simba kwa njia ya penati
dakika ya 19 lililofungwa na mchezaji Deogratius Julius baada ya
mchezaji wa Simba Donald Musoti kuunawa mpira katika eneo la adhabu.
Hata
hivyo wachezaji wa timu ya Simba walimzonga mwamuzi wa mchezo huo
Mathew Akrama aliyepuliza filimbi ya kuashiria penati hali ambayo
ilisababisha mpira usimame
kwa dakika kadhaa ambapo hata hivyo mpira wa adhabu ulipigwa na
mchezaji Julius na kumuacha golikipa Yaw Beko akichupa bila mafanikio.
Hadi
mapumziko Mbeya City ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0.Kipindi cha pili
kilianza kwa kila timu kuingia kwa kasi ambapo mpira ulikuwa ni wa
kushambuliana kwa pande zote.
Ilikuwa
ni dakika ya 52 mchezaji wA Simba Said Ndemla aliwainua mashabiki wa
timu hiyo baada ya kuipatia timu yake bao la kusawazisha baada ya
golikipa wa timu ya Mbeya City David Burhan kutoka golini na kumpa
nafasi Ndemla kufunga bao kufuatia pasi kutoka kwa Hamis Tambwe.
Mbeya City
David Burhani, John Kabanda,Hamad Kibopile,Deogratius Julius,Y usuf Abdallah,Antony Matogolo,Peter Mapunda,Steven Mazanda,Paul Nonga,Hassan Mwasapili na Deus Kaseke.
SIMBA
Yaw Beko, William Lucian,Henry Joseph,Joseph Owino,Dolnad Musoti,Jonas
Mkude,Amri Kiemba, Said Ndemla,Hamis Tambwe,Ramadhan Singano na Harun Chanongo.
Post a Comment