BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
UFAFANUZI
WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA
NNE (CSEE) 2013
Imetolewa Na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
25 Februari, 2014
UFAFANUZI
WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA
NNE (CSEE) 2013
Baraza la Mitihani la
Tanzania lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013 tarehe 21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa
matokeo hayo, Baraza limekuwa likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa
baadhi ya wadau wa elimu hawakuelewa vizuri kuhusu Viwango vya Ufaulu (grade ranges), alama ya chini ya ufaulu (pass mark) na Ufaulu wa jumla wa mtahiniwa (overall performance). Baraza la
Mitihani linapenda kutoa ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo:
1.
Viwango vya ufaulu (grade ranges) ni makundi
ya alama yanayopangwa ili kuwaweka pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika
somo husika na kuwatofautisha na watahiniwa waliopo katika kundi jingine. Makundi
haya hupangwa ili kuwawezesha wadau kutambua namna watahiniwa walivyotawanyika
katika viwango mbalimbali vya umahiri wa somo husika. Baraza la Mitihani la
Tanzania, limekuwa likitumia makundi Matano (5) kwa kipindi kirefu hadi mwaka
2012. Aidha, Kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013, Baraza limeanza kutumia utaratibu wa Makundi Saba (7) ambayo ni A, B+, B, C, D, E na F. Utaratibu huu umelenga kupunguza mlundikano
mkubwa wa alama katika kundi moja. Mgawanyo wa makundi hayo ni kama
inavyoonekana kwenye Jedwali la 1.
Jedwali
Na 1: Viwango vya ufaulu vilivyotumika katika Matokeo ya CSEE 2013.
Kundi
|
Gredi
|
Alama
|
Idadi ya Pointi
|
1
|
A
|
75 - 100
|
1
|
2
|
B+
|
60 - 74
|
2
|
3
|
B
|
50 - 59
|
3
|
4
|
C
|
40 - 49
|
4
|
5
|
D
|
30 - 39
|
5
|
6
|
E
|
20 - 29
|
6
|
7
|
F
|
0 - 19
|
7
|
Aidha, Idadi ya makundi ya ufaulu hutofautiana
kati ya nchi na nchi kulingana na mahitaji ya nchi husika. Kwa mfano; Kenya wana makundi Kumi na mbili
(12), Malawi Tisa (9), Uganda Tisa (9), Nchi za Afrika magharibi (Nigeria,
Ghana, Siera Leone na Liberia) makundi Tisa.
2.
Kwa kuzingatia viwango vya ufaulu
vilivyoainishwa katika makundi saba yaliyopo kwenye Jedwali na 1, kiwango cha
chini cha ufaulu ni gredi D na kiwango cha juu cha ufaulu ni Gredi A. Mtahiniwa
atakuwa amefaulu somo husika iwapo atapata gredi D na kuendelea. Aidha,
mtahiniwa aliyepata gredi E na F atakuwa hajafaulu somo husika.
3.
Madaraja ya ufaulu yamepangwa kwa mujibu wa kifungu
cha 20 (1)-(6) cha Kanuni za Mitihani kinachoelekeza kuwa Ufaulu katika daraja
la Kwanza hadi la Tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama (Points) na Ufaulu
katika Daraja la Nne unapangwa kwa
kuzingatia ufaulu wa chini aliopata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo
yasiyopungua mawili au ufaulu kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C katika
somo moja. Hivyo, madaraja yaliyotumika ni kama yanavyoonekana kwenye Jedwali la
2.
Jedwali 2: Madaraja
yaliyotumika katika CSEE 2013
Daraja
|
Pointi
|
I
|
7 – 17
|
II
|
18 – 24
|
III
|
25 – 31
|
IV
|
1.
Ufaulu katika somo moja kwa kiwango kisichokuwa chini
ya Gredi C au
2.
Ufaulu katika masomo yasiyopungua mawili katika Gredi D
|
0
|
Alama chini ya D
mbili
|
4.
Kwa mujibu wa Kanuni za Mitihani, ufaulu wa
somo katika Gredi A hadi C utakuwa ni ufaulu wa “Credit” na Gredi D itahesabika
kuwa ni “pass”. Aidha Gredi E na F zitakuwa alama za kufeli.
5.
Baraza la mitihani la Tanzania linapenda kutoa
taarifa kwamba ufafanuzi wa sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali
kwa kutumia mfumo huu mpya wa madaraja utatolewa na mamlaka husika ambapo
Kamishna wa Elimu atalitolea ufafanuzi zaidi.
Imetolewa Na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
PROMO DELIMA
ReplyDeletepoker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya
Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%
Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!
Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845