Rais Kikwete kabla ya kuanza matembezi leo asubuhi eneo la Soweto Jijini Mbeya. |
Mwenyekiti wa CCM Taifa akisalimiana na Makamu Mwenyekiti mara kabla ya kuanza matembezi ya mshikamano leo asubuhi. |
Rais Kikwete akiwasili katika eneo la Soweto kwa ajili ya kuanza matembezi ya Mshikamano. |
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika magari mawili ya Polisi wakichukua matukio wakati wa matembezi ya mshikamano leo asubuhi |
Rais Kikwete na Mwenyekiti wa CCM Taifa akizungumza na wananchi mara baada ya kumaliza matembezi ya mshikamano katika Bustani ya Jiji la Mbeya leo asubuhi. |
MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete leo ameongoza matembezi ya mshikamano Jijini Mbeya kwa kutembea umbali wa kilomita 2 kutoka eneo la Soweto hadi Uwanja wa Sokoine.
Matembezi hayo ya mshikamano yameambatana na maadhimisho ya miaka 37 tangu kuzaliwa kwa chama hicho Februari 5 1977 ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Mbeya katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine leo mchana.
Rais Kikwete ambaye aliambatana na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana, Waziri wa Rais Kazi Maalum Prof Mark Mwandosya, Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Godfrey Zambi, Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Mchemba,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa na Taifa.
Matembezi hayo ambayo yalianza majira ya saa 1:00 asubuhi yameishia katika Bustani ya Jiji la Mbeya iliyopo karibu na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ambapo Rais Kikwete aliungana na mamia ya wananchi kutembea bila kuchoka.
Katika maandamano hayo Rais Kikwete aliwachukua watoto wanne na kuongozana nao hadi mwisho wa matembezi ambapo baadaye aliwataka wanausalama kuchukua majina ya watoto hao na kumkabidhi.
Tofauti na ilivyokuwa katika miaka ya nyuma eneo la Soweto,Kabwe na Mwanjewa ambako mara nyingi kumekuwa na historia ya vurugu, baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wa maeneo hayo walijitokeza kwa uchache na kupungia mkono matembezi hayo bila vurugu zozote.
Post a Comment