Ads (728x90)

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata hivi punde katika habari mpasuko ya Radio One kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi kwamba, Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa ITV na Radio One Stereo Ufoo Saro amejeruhiwa kwa kupigwa risasi baada ya kuvamiwa na mtu asiyefahamika nyumbani kwake Kibamba Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Aidha mvamizi huyo alimuua mama yake Ufoo papo hapo na yeye mwenyewe kujiua kwa risasi, (chanzo Radio One Stereo)
Ufoo Saro akiwa na waandishi wenzake wa chombo chake Festo Sikagonamo na Danny Tweve wakati wa maadhimisho ya siku ya Mei Day ambayo yalifanyika Kitaifa katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya mwaka huu.

Post a Comment