Ads (728x90)


TIMU 36 za kata zinatarajia kuchuana kumtafuta bingwa atakayewakilisha Jiji la Mbeya  katika michuano ya kombe la Pepsi Meyors Cup linalodhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya SBC mkoani Mbeya.
Akizungumza Jijini Mbeya mratibu wa mashindano hayo Mkurugenzi wa kampuni ya Myway Entertainment Paul Mganga alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kuchezwa kwa mtindo wa mtoano kwa awamu ya kwanza kabla ya kuzikutanisha timu 18 ambazo zitacheza kwa mtindo wa ligi.
Alisema kuwa mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Kampuni ya vinywaji baridi vya Pepsi SBC itagawanywa katika makundi 6 ambazo zitajumuisha jumla ya kata 36 katika viwanja 6.
Mganga alizitaja timu zitakazoshiriki kuwa ni Iduda, Uyole, Nsalaga,Igawilo, Iganjo,Itezi, Ilomba, Mwasanga, Mwakibete,Ilemi, Tembela,Isyesye, Isanga, Itagano, Ruanda, Mwansekwa, Iyela,Iganzo.
Zingine ni timu za Mbalizi Road,Sinde,Forest, Mabatini, Sisimba,Maanga, Maendeleo, Iziwa, Ghana, Nonde, Nsoho, Itiji, Iwambi, Nzovwe, Iyunga, Kalobe na Itende.
Alisema kuwa mshindi wa kwanza katika ligi hiyo ataondoka na kitita cha sh. milioni 5 ikiwa ni Bajaj yenye thamani ya sh. milioni 4 pamoja na fedha taslimu sh. milioni 1 ambapo mshindi wa pili ataondoka na sh. milioni 1.5 ilhali mshindi wa tatu atajinyakulia jumla ya sh. 500,000.
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga alisema kuwa mashindano hayo yatasaidia kuibua vipaji kutoka kwa wachezaji wa timu za mitaani ambao watapata fursa ya kuichezea timu ya ligi kuu ya Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SBC Jacques Pretorius alisema kuwa kampuni yake imejitolea kudhamini ligi hiyo kutokana na umuhimu wake wa kurejesha huduma kwa walaji wa vinywaji vinavyozalishwa na kampuni hiyo.


Meneja Mkuu wa Kampuni ya SBS inayozalisha vinywaji vya Pepsi Jacques Pretorius akielezea mchango wa kampuni hiyo katika masuala ya michezo duniani.Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakijumuika katika uzinduzi wa ufadhili wa Kampuni ya SBC kudhamini kombe la Meya Jijini Mbeya.

Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Mussa Zungiza akielezea umuhimu wa ufadhili wa Pepsi kwa kombe la Meya Jijini Mbeya.

Mratibu Mashindano ya Kombe la Meya Paul Mganga kampuni ya Myway akizungumzia utaratibu wa mashindano ya Meya Jijini Mbeya.


Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga akishukuru udhamini wa kampuni SBC juu ya mashindano ya Meya.


Mratibu wa mashindano ya Kombe la Meya Paul Mganga akizungumza ratiba ya mashindano.

Meya wa Jiji la Mbeya akipongezana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya SBC baada ya kukubali kudhamini mashindano ya kombe la Meya.

Post a Comment