Ads (728x90)

Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia ushindi kwa staili ya aina yake baada ya kuibuka kidedea dhidi ya kaka zao Prison kwa bao 2-0 kwenye uwanja wa Sokoine leo jioni
Wachezaji wa Mbeya City wakitoa ishara kwa mashabiki wao kabla ya mechi kati yao na Prison kuanza
Ni furaha tupu baada ya ushindi dhidi ya kaka zao wa Prison
Mchezaji wa Mbeya City Deus Kaseke akiwa ameanguka chini baada ya kuvutwa shati na mchezaji wa Prison Laurian Mpalule anayekimbilia mpira
Mwamuzi wa mchezo huo Irael Nkongo akimzawadia kadi ya njano mchezaji wa Prison Laurian Mpalule baada ya kuvuta shati mchezaji wa Mbeya City Deus Kaseke, mwamuzi alitoa adhabu ya penati dhidi ya Prison na kusababisha goli la pili lililofungwa na Deogratius Julius
Golikipa wa Prison Beno Kakolanya akiuangalia mpira ukiwa umetinga wavuni baada ya Deogratius Julius kupachika bao hilo kwa njia ya Penati
Mbeya City wakishangilia ushindi
Mashabiki wa Mbeya City wakishangilia ushindi dhidi ya timu yao
Ni furaha nderemo na vifijo katika uwanja wa Sokoine
Wachezaji wa Mbeya City kabla ya kuanza kwa mchezo kati yao na kaka zao maafande wa Prison
Mashabiki wa Mbeya City wakiwatambia wenzao mashabiki wa Prison kabla ya kuanza kwa mechi hiyo
Nao mashabiki wa Prison wakiwatambia wenzao wa Mbeya City kabla ya mechi kuanza
Mashabiki wa Mbeya City wakiwa wamebeba jeneza lenye bendera ya Prison mara baada ya kushinda
Kocha wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi akiwa haamini macho yake baada ya timu yake kufanya vyema katika mechi hiyo
Wachezaji wa Mbeya City kabla ya mchezo

Wachezaji wa Prison kabla ya mechi na Mbeya City
Goli la kwanza la Mbeya City lilivyoingiaLIGI kuu ya Tanzania Bara leo imeendelea katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya,ambapo timu ya Mbeya City imewaonesha ubabe kaka zao wa Prison kwa kuwatandika bao 2-0.
Timu hizo zimekutana kwa mara ya kwanza baada ya Mbeya City kupanda daraja na kutoa hisia za kipekee miongoni mwa wapenzi wa soka Jijini Mbeya.
Mechi hiyo ambayo ilionesha kuwa na upinzani mkubwa ilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu ambapo katika kipindi cha kwanza Prison walionesha kutumia uzoefu na ukongwe wao katika ligi kuu kwa  kumiliki mpira kwa muda mrefu.
Hata hivyo pamoja na kumiliki mpira kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka uwanjani bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikiwania kupata goli la ushindi ambapo katika dakika ya 62 mchezaji wa timu ya Mbeya City Peter Mapunda aliyeingia kipindi cha pili badala ya Alex Sethi aliwainua mashabiki wa Mbeya City kwa kupachika bao safi baada ya kupiga shuti lililoshindwa kuzuiwa na walinzi wa Prison.
Goli hilo liliamsha shamrashamra uwanja mzima ambapo wachezaji wa timu ya Prison walionekana kuchanganyikiwa na kujikuta wakicheza rafu na kusababisha goli lililofungwa kwa njia ya penati dakika 67 na mchezaji Deogratius Julius.
Mwamuzi wa mchezo huo Israel Nkongo alitoa adhabu hiyo baada ya mchezaji wa Prison Laurian Mpalule kumvuta shati mchezaji wa Mbeya City Deus Kaseke ambaye alikuwa akikata mbuga kuelekea katika lango la Prison na kusababisha refarii kutoa penati sanjari na kadi ya njano kwa mchezaji wa Prison Laurian Mpalule.
Hadi Kipyenga cha mwisho kinapulizwa Mbeya City ilikuwa mbele kwa Bao 2-0, Tofauti na mechi zingine uwanja wa Sokoine ulifurika mashabiki na kutoa hamasa ya kipekee kwa mchezo huo ambao awali uliibua gumzo na hisia kwa wakazi wa Jiji la Mbeya.
Mbeya City iliwakilishwa na wachezaji David Burhani,John Kapande,Hassan Mwasapili,Deogratius Julius,Yusuf Abdallah,Antony Matogolo,Alex Seth/Peter Mapunda,Steven Mazanda,Paul Nonga, Jeremia John na Deus Kaseke,
Prison iliwakilishwa  na Beno Kakolanya,Salum Kimenya,Boniface Hau,Jumanne Elfadhili,Lugano Mwangama,Jimmy Shoji,Jeremia Juma,Fred Chudu,Omega Seme,Ibrahim  Isack na Peter Michael.
Waamuzi katika mechi hiyo walikuwa ni Israel Nkongo (Dar)Samwel Mpenzu (Arusha)Mohamed Mkono (Tanga) na  Mirambo Shikungu(Mbeya)

Post a Comment