Jeraha katika mguu wa mwandishi wa habari Shomi Mtaki lililotokana na risasi baada ya kuvamiwa na majambazi |
Shomi Mtaki akionesha jeraha lililotokana na risasi katika mguu wake wa kushoto |
Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One wilayani Mbozi Danny Tweve alipomtembelea Shomi Mtaki kumjulia hali baada ya kuvamiwa na majambazi na kujeruhiwa kwa risasi |
Mke wa Shomi Mtaki ambaye naye alijeruhiwa na baruti kifuani kwake |
Sehemu ambayo risasi ilipigwa katika mlango |
Namna ambavyo majambazi yalivyofanya upekuzi katika chumba cha Mtaki kutafuta fedha walizodhani kuwa amehifadhi |
Shomi Mtaki aliyejeruhiwa kwa kipigwa risasi na majambazi |
Ndugu na jamaa wakiifariji familia ya Mtaki baada ya tukio hilo la uvamizi na kupigwa risasi |
Kamanda wa Polisi wilaya ya Momba Bw. Chitanda akimpa pole Shomi Mtaki |
Nyumba na trekta katika shambani kwa Shomi Mtaki katika mji mdogo wa Mpemba Tunduma wilayani Momba |
NI wiki ya majanga kwa waandishi wa
habari nchini, muda mfupi baada ya kupata taarifa ya kupigwa risasi kwa Mwandishi
wa habari wa ITV /Radio One Mwandishi mwingine wa gazeti la Uhuru mjini Tunduma
wilayani Momba mkoani Mbeya Shomi Mtaki amepigwa risasi baada ya kuvamiwa
na majambazi shambani kwake katika mji mdogo wa Mpemba.
Mtaki ambaye alikuwa katika nyumba
iliyopo shambani kwake alivamiwa usiku wa Octoba 10 na watu watano waliokuwa na
silaha aina ya bunduki kisha kumlazimisha kutoa fedha.
Wanablogu waliomtembelea shambani
kwake walishuhudia majeraha aliyokuwa nayo Mtaki katika maeneo mbalimbali ya
mwili wake ambapo alisema kuwa siku hiyo majira ya saa 9:00 usiku alisikia
mchakato wa miguu nje ya nyumba yake na kwamba alipochungulia aliwaona vivuli
vya watu wakiwa wamesimama karibu na trekta lake nje ya nyumba.
Alisema kuwa alipowashitua watu hao
walitamka wazi wazi kuwa wanataka fedha na muda huo huo akasikia kishindo
kikubwa katika mlango wa kuingilia sebuleni ambapo wavamizi hao walikuwa
wamepiga jiwe aina ya FATUMA kwa lengo la kuuvunja mlango ili waingie ndani.
Alisema kuwa mara akasikia mlio wa
risasi ikipigwa katika mlango wake na mara ukafunguka na vijana watatu
waliingia sebuleni ambapo walichukua jiwe walilotumia kuvunja mlango wa
sebuleni na kupiga katika mlango wa chumbani na kisha baadaye walimimina risasi
katika mlango huo ambazo zilimpata katika mguu wa kushoto na kumjeruhi.
Mtaki alisema kuwa yeye na mkewe
walikuwa wakihangaika na kujaribu kujiokoa maisha yao ambapo mkewe aliposikia
mlio wa risasi aliingia chini ya mvungu wa kitanda ili kujinusuru.
‘’Nilijiona nakikaribia kifo vijana
walimimina risasi katika mlango wa chumbani zikanikuta mguuni na kunijeruhi
vibaya, mlango ukafunguka wakaingia vijana watatu ambao hawakujiziba sura zao,’’alisema.
Alisema kuwa mara baada ya kuingia
walianza kumuamrisha atoe fedha, akawajibu kuwa hana fedha ndipo walipoanza
kumpiga mgongoni huku wakitishia kumuua na kwamba wakati huo mkewe alikuwa
amejificha katika mvungu wa kitanda.
‘’Wale wavamizi walianza kupekuwa
vitu mbalimbali, wakachukua simu yangu ya mkononi ambayo mtu wa mwisho
kuwasiliana naye alikuwa ni shemeji yangu ambaye ni Mwanajeshi,’’alisema na
kuongeza.
‘’Wavamizi wale walichukua simu tatu,
simu moja ikajipiga kwa bahati shemeji yangu aliipokea, akasikia vurumai iliyokuwa
ikiendelea nyumbani na namna ambavyo tulivyokuwa tukijitetea ili tusiuawe, muda
huo huo akaenda kutoa taarifa polisi,’’alisema.
Alisema kuwa wavamizi hao waliingia
katika mji wake majira ya saa 8:45 na kuendelea kuwepo pale hadi majira ya saa
9;00 usiku ambapo walichukua simu tatu, tv seat ya nchi 22, ving’amuzi viwili
kimoja cha Startimes na kingine cha Zuku vyote vikiwa na thamani ya sh. Milioni
2.
Alisema kuwa mara baada ya wavamizi
hao kumaliza kukusanya vitu walivyoona vinafaa waliwaamrisha kuingia chumbani
na wao wakatokomea upande wa mashariki na muda mfupi baadaye polisi walifika
eneo la tukio wakatukuta mien a mke wangu tukiwa tumekumbatiana huku tukilia na
kumuomba Mungu.
Post a Comment