Ads (728x90)


Kwa niaba yetu mimi na familia yangu, tunawatakia Eid Mubarak ndugu jamaa na marafiki, tunawapa mkono wa Eid,tunawapenda nyoote tunatoa shukurani ya kuendelea kutuunga mkono na kutusapot kwa fikra mawazo na hata kutupa moyo katika maisha ya kila siku.
Tunaamini kila binadamu anakumbwa na matatizo na majanga ya kimaisha kila siku, kuna wakati hukata tamaa na kujikuta akitarazia kufanya mambo ya yasiyo ya kawaida, wengine hujitokeza na kutoa ushauri wa namna moja ama nyingine kwa nia ya kujenga familia.
yapo mengi yanayotukumba katika maisha bali ushauri wa kibinadamu huleta matumaini na faraja na kuifanya dunia endelee kuwepo na watu wake waendelee kuishi kwa amani na Utulivu.
 Hatuna cha kuwapa bali tunawaombea kwa Mungu azidi kuwapa umri mrefu ili muendelee kutushauri pale tunapoteleza na hata kukosea!!!
Aidha tunatumia fursa ya siku hii ya leo kuwaomba msamaha wale wote tuliowakosea kwa namna moja ama nyingine, makosa yangu au ya wale wanaonihusu kwenu si ya kukusudia bali yanatokana na hulka za kimaumbile.
Nachakua fursa hii kuwaomba radhi kwa yote ili tufungue ukurasa mpya wa maisha ya amani faraja na utulivu, tukumbuke kuwa kuna siku tutaicha hii dunia tutaulizwa mbele ya Mungu wale waliotukosea tuliwasamehe ama tuliwawekea inda ya milele, NAWAPENDA WOTE NAWATAKIA EID EL HAJ NJEMA KARIBUNI NYUMBANI!!!!

Post a Comment