Ads (728x90)

Uharibifu na uchomaji wa moto katika vurugu Jijini Mbeya uliharibu miundo mbinu na kuingiza hasara ya sh. milioni 20

Kusimama kwa shughuli za Biashara katika vurugu Jijini Mbeya kulisababisha hasara ya sh. bilioni 2.6

Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara na Viwanda mkoa wa Mbeya TCCIA Julius Kaijage akitoa tathmini ya vurugu za Jiji la Mbeya zilizofanyika mwanzoni mwa mwezi Oktoba.



VURUGU zilizotokana na watu   wanaodaiwa kuwa ni wafanyabiashara wa Jiji la Mbeya zilizotokea mwanzoni mwa mwezi huu zimedaiwa kusababisha hasara ya zaidi ya sh. bilioni 2 ikiwemo uharibifu wa mali za umma, uchomaji wa barabara na kusimama kwa biashara.
Wakizungumza katika kikao maalumu kilichohusisha, Jeshi la polisi, wafanyabiashara, wananchi na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara na viwanda TCCIA Julius Kaijage walisema hasara iliyotokana na vurugu hizo ni sh. bilioni 2.26.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Kandoro alisema kuwa tathmini iliyofanywa baada ya vurugu hizo kutokea utaigharimu serikali jumla ya sh. milioni 20 fedha ambazo zingeweza kusaidia huduma zingine za kijamii kama vile elimu na afya.
Alisema kuwa wananchi wa Jiji la Mbeya wanapaswa kujua kuwa vurugu zozote zinazoambatana na uharibifu wa mali ya umma hauna tija kwao kwa kuwa unasababisha serikali kuingia gharama za matengenezo fedha ambazo ni za walipa kodi.
‘’Ifike mahala wananchi wanapaswa kujua kuwa hasara inayotokea inatugharimu sote, fedha hizi ni za walipa kodi ambao ni mimi na wewe, tunapofanya uharibifu tunajirudisha nyuma wenyewe,’’alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TCCIA Bw.Kaijage alisema kuwa kwa siku mbili ambazo wafanyabiashara, wamachinga na akina mama Lishe walifunga biashara kutokana na mgogoro kati yao na Mamlaka ya Mapato TRA umesababisha hasara ya zaidi ya sh bilioni 2.6.
Alisema ili kukabiliana na hali ya uvunjifu wa amani unaotokana na watu wanaodaiwa kuwa ni wafanyabiashara TCCIA imeandaa makubaliano maalumu ya kuunda kamati za ulinzi katika maeneo ya biashara.

Post a Comment