Ads (728x90)

Siku Nyenyembe alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Jijini Dar

Akisaidiwa na wauguzi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Jijini Dar,Picha chini baadhi ya waandishi wa habari wa Jijini Dar es salaam waliojitokeza kumpokea Nyenyembe katika uwanja wa ndege wa Kimataifa alipotokea Mbeya.
Gari la Wagonjwa lililombeba Nyenyembe kutoka Uwanja wa Ndege hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili (PICHA KWA HISANI YA FACEBOOK YA KENETHY NGELESI)

.'Ndugu Zangu Waandishi wa Habari na wadau wengine wa habari nawashukuru kwa maombi na dua zenu, Mwenyezi Mungu anaendelea kunipa afya njema na ninaendelea na matibabu, leo hii naenda kufanya check up nipo hapa Muhimbili Hospitali, nashukuru kwa kunipigia ndugu yangu Rashid, vipi harakati zinaendeleaje huko Mbeya?
 Ni sauti ya Mwandishi wa habari na Mwenyekiti Mstaafu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya Christopher Nyenyembe alipokuwa akiongea nami kwa njia ya simu muda mfupi uliopita, nimefarijika kusikia sauti yake yenye nguvu isiyo na mikwaruzo kama ilivvyokuwa hapo awali, akizungumza kwa matumaini huku akileta utani wake wa kawaida, ni faraja kubwa na ni fursa pekee ya kumshukuru Mwenyezi Mungu muweza wa yote ambaye alipangalo ndilo huwa, Nyenyembe mpiganaji, mwanahabari mkongwe, mshairi na mchambuzi wa mambo mbalimbali ya kijamii,uchumi na siasa sasa hivi yupo feet na anaendelea vyema kiafya.


Post a Comment