Ads (728x90)

Mabadiliko ya Tabia nchi na Athari zake na matumzi mabaya ya ardhi  huathiri mazingira
Wanavijiji wanapaswa kupewa elimu ya mara kwa mara juu ya mabadiliko ya Tabia nchi na Athari za Mazingira ili waweze kukabiliana na hali halisi ya mabadiliko.
Asasi za Kiraia na taasisiz a kiserikali zina majukumu makubwa ya kuelimisha umma katika majadiliano ya pamoja ambayo huibua changamoto ambazo hatimaye unapatikana ufumbuzi juu ya matatizo yatokanayo na uharibifu wa mazingira

Athari itokanayo na mabdiliko ya Tabia nchi huvikumba vizazi na athari yake itaonekana baada ya miaka mingo ijayo, urithi wa baadaye kwa vizazi vijavyo hutegemea maandalizi bora kwa vizazi vya sasa
Elimu Shirikishi kwa matumizi bora mimea na uoto wa asili huwazindua wananchi
Wanafunzi katika shule za Msingi wanapaswa kuelimisha namna ya utunzaji wa mazingira kwa manufaa yao siku za usoni
Zamani wazee walijitahidi kuhifadhi miti ya asili na kuitunza hata vizazi vya sasa vikaikuta miti hiyo ambayo hutumiwa kwa ajili ya vivuli, matunda na uhifadhi wa maji katika vyanzo vya mito
Dhana shirikishi kwa mchango kati ya Assasi za Kiraia na Watendaji wa serikali itasaidia kuleta ufumbuzi wa matatizo ya uharibifu wa mazingira

Jamii za wafugaji na wakulima wanao mchango mkubwa kufanikisha tatizo la uharibifu wa mazingira linatoweka nchini

Post a Comment