Ads (728x90)

Wachezaji wa Timu ya JKT Ruvu wakiingia uwanjani kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu kati yake na timu ya Mbeya City kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya

Mashabiki wa timu ya JKT wakiingia uwanjani kuishangilia timu yao
Mashabiki wa timu ya JKT Ruvu wakishangilia timu yao
Washawasha la polisi nalo lilikuwa mstari wa mbele kuhakikisha hali ya usalama inadumishwa katika mechi kati ya Mbeya City na JKT Ruvu

Mashambulizi langoni mwa JKT Ruvu


Mlinzi wa JKT Ruvu  Kesi Mapande akimzuia mshambuliaji wa Mbeya City  Deus Kaseke wakati wa patashika langoni mwa timu ya JKT Ruvu

Mchezaji wa timu ya Mbeya City akigalagala chini baada kuumia huku wachezaji wa timu ya JKT Ruvu Kesi Mapande na Nashon Naftal wakiwa wamesimama pembeni
Kikosi cha timu ya Mbeya City kilichowapigisha kwata JKT Ruvu uwanja wa Sokoine leo jioni

Wachezaji wa timu ya JKT Ruvu wakiwasalimia wachezaji wa Mbeya City kabla ya kuanza kwa mchezo
Kikosi cha timu ya JKT Ruvu kabla ya mechi kati yao na timu ya Mbeya City leo jioni
Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe naye alikuwa mmoja wa watazamaji wa timu mechi kati ya Mbeya City na JKT Ruvu


 
 
TIMU ya Mbeya City ya Jijini Mbeya imeendelea kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kuitandika timu ya JKT Ruvu bao 1-0, bao lililopatikana dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku kila timu ikiwania kupata bao la kuongoza ambapo golikipa wa timu ya JKT Ruvu alionekana kufanya kazi kubwa kwa kuondosha mara kwa mara mipira iliyoelekezwa langoni mwa timu yake.

Goli la Mbeya City  lilipatikana dakika ya 36 baada ya mchezaji Jeremia John kuwatoka walinzi wa timu ya JKT Ruvu Mussa Zuberi, Kesi Mapande na Omar Mtaki na kupiga bao safi lililomwacha kipa wa JKT Ruvu Shaaban Dihile akichupa bila mafanikio.
 
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mbeya City ilitoka kifua mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikilishambulia bao la mpinzani wake,timu ya Mbeya City ilionekana kuutawala zaidi mchezo dhidi ya JKT Ruvu, hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi  Antony Kayombo kutoka mkoani Rukwa kinapulizwa Mbeya City ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0.

Post a Comment