Ads (728x90)

Wachezaji wa Mbeya City hujituma   na hata kujitoa mhanga ili kupigania ushindi wa timu yao.
Bango linaloonesha Majigambo ya Mashabiki wa Mbeya City dhidi ya timu zinazoingia Mbeya kucheza na timu hiyo linalosomeka ''UKIINGIA MBEYA HUTOKI''
Wachezaji wa timu ya Mbeya City wakiwaelekea mashabiki baada ya mechi kuwashukuru kwa sapoti yao.
Wachezaji wa Mbeya City wakitoka kupata baraka za mashabiki wao katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kikosi cha Mbeya City kilichoitoa jasho timu kongwe ya Coastal Union ya Tanga.
Kikosi cha Mbeya City kilichowachezesha kwata JKT Ruvu mwishoni mwa wiki.
Kikosi cha JKT Ruvu kilichocheza na Mbeya City mwishoni mwa wiki na kufungwa bao 1-0 katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.
Wachezaji wa Timu ya Mbeya City wakifurahia ushindi na kuwashukuru mashabiki kwa sapoti yao katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.


-Ina uwezo mkubwa kimchezo,nidhamu na kujituma ni sehemu ya mafanikio yao katika ligi Kuu. 

Na Rashid Mkwinda
SIRI ya majigambo na  ushindi wa timu ya Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambayo imepanda daraja na kucheza Ligi Kuu na hatimaye kuwa tishio kwa timu zote zinazocheza ligi hiyo nchini imebainika.
Timu hiyo inayoongozwa na Mwalimu Juma Mwambusi imejichukulia sifa lukuki ambapo awali ilionekana kana kwamba inacheza kwa nguvu ya soda huku baadhi ya viongozi wa timu ilizowahi kucheza nazo walwahi kuibeza wakidai kuwa timu hiyo inacheza kwa sifa haiwezi kufika mbali kisoka.
Kejeli aina hiyo ziliwahi kutolewa na kocha wa timu ya Coastal Union ya Tanga ...na Msemaji wa timu ya Yanga Baraka Kizuguto ambapo kocha wa timu ya Coastal Ally Kidi alisema kuwa majukumu inayopewa timu hiyo ni makubwa kuliko uwezo wake hivyo haiwezi kufika mbali ilhali msemaji wa timu ya Yanga Baraka Kizuguto aliisifia timu hiyo kwa kusema kuwa iwapo ikipata maandalizi ya kutosha inaweza kuwa timu nzuri ijapokuwa inavurugwa na mashabiki wake wanaoshangilia kupita kiasi na hata kusababisha vurugu.
Matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Yanga yalibezwa huku timu hiyo ikikamiwa kwamba ikicheza nje ya uwanja wa nyumbani inaweza kufungwa magoli mengi kwa kuwa haina mashabiki, jibu la maswali hayo lilipatikana katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Taifa dhidi ya Timu ya Simba ambapo iliilazimisha sare ya mabao 2-2 timu hiyo kongwe na kuwaacha midomo wazi mashabiki lukuki waliofurika katika uwanja wa Taifa juu ya uwezo wa timu hiyo changa na ngeni katika ligi Kuu.
Kinachoonekana katika timu hiyo ni uwezo wao wa kutumia vyema mafundisho ya kocha wa timu yao Juma Mwambusi sanjari na  kujituma kwa wachezaji hao wakiiamini mashabiki ni sehemu ya ushindi wa timu wao.
Pamoja na mashabiki wa timu ya Mbeya City kufanya vitendo vilivyowaudhi timu ya Yanga walipokuwa Jijini Mbeya kwa kuvunja kioo cha Basi lao na hata kumjeruhi dereva wa gari hilo,waliweza kuwateka mashabiki wa timu ya Yanga katika uwanja wa Taifa pale wachezaji hao waliposhikana mikono na kwenda upande wa jukwaa la mashabiki wa Yanga na kuonesha dalili za kuomba radhi kufuatia tukio lililotokea mkoani Mbeya.
Kitendo hicho kiliamsha hisia kali za uungwana zilizofanywa na vijana hao chipukizi na hata kuonesha kuwa ni vijana wenye displin katika mchezo na kwamba kilichotokea Mbeya hakikukusudiwa na wachezaji hao bali ni cha wahuni wachache waliotumia fursa hiyo kutaka kuwavurugia mustakabali wao katika ligi kuu.
Mbeya City ambayo kwa sasa iko nafasi ya pili nyuma ya Azama FC ikiwa na pointi 20 imeendelea kuutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kujitahidi kushinda katika kila mechi inayocheza nyumbani na kuendelea kuwapa raha mashabiki wake wa mkoa wa Mbeya waliotokea kuipenda na kuiunga mkono timu hiyo kwa hali na mali.
Kila timu iko na siri yake ya ushindi, ushindi wa timu unatokana na uwezo mkubwa wa kujituma kwa wachezaji hao kuanzia kipindi cha kwanza hadi kipindi cha mwisho bila kuchoka, nidhamu katika mchezo na mapenzi waliyonayo miongoni mwao na hata  kukubali kukosolewa pale wanapoonekana wanakosea.
Kikubwa zaidi ambacho kimeonekana kuwavutia wapenzi na mashabiki wengi wa mkoa wa Mbeya ni desturi yao ya kuwakubali mashabiki wao ambapo wameweza kuiteka hadhira ya kila mpenzi wa mpira wa miguu Jijini Mbeya, kabla ya kuanza kwa mchezo wachezaji hao kwa pamoja hujikusanya na kuwaelekea mashabiki wake na kuwapungia mkono na kuomba baraka zao na hata wanapomaliza mchezo hufanya vivyo hivyo ambapo nderemo vifijo na vigelegele huendelea kuanzia mwanzo wa mechi hadi kipyenga cha mwisho kinapopigwa na mwamuzi wa mechi hiyo.
Kikosi cha timu ya Mbeya City kinaundwa na David Burhani, John Kabanda,Hamad Kibopile, Yusuf Abdallah,Deogratius Julius,Antony Matogolo,Deus Kaseke,Steven Mazanda,Paul Nonga, Jeremiah John,Francis Castor, Jofrey Jackkson,Baraka Haule, Richard Brown, Yohana Moris, Mwagane Yeya, Richard Peter na Peter Mapunda wakiwa chini ya Mwalimu Juma Mwambusi na msaidizi wake  Maka Mwalwisi.



Post a Comment