Ads (728x90)DIWANI WA KATA YA KIWIRA ADAIWA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI....
Diwani wa Kata ya Kiwira Wilayani Rungwe, Lawland Mwakalibule leo amekamatwa akituhumiwa kufanya mapenzi na mwanafunzi anayesoma katika Shule ya Sekondari Kiwira, kidato cha Tatu. Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Binti huyo alitoweka nyumbani kwao tokea jana, mpaka aliporejea leo asubuhi, wazazi wake walipombana awaeleze wapi alilala usiku wa leo ndipo aliposema kuwa alilala na Mhe. Diwani Lawland Mwakalibule.Baada ya kupata maelezo hayo wazazi wa mwanafunzi huyu walichukua hatua ya kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Kiwira. Polisi walichukua hatua ya kumtafuta diwani Mwakalibule na kumuweka chini ya ulinzi wakati upelelezi wa tukio hili ukiendelea. Mtuhumiwa kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Rungwe mjini Tukuyu.Mpaka mwandishi wetu anatoka katika kituo cha polisi mjini Tukuyu mtoto wa shule alikuwa amepelekwa hospitali ya Wilaya ya Rungwe 'Makandana' kwa uchunguzi zaidi wa kitaalamu.

 
Diwani wa Kata ya Kiwira Lawland Mwakalibule akiwa katika kituo cha Polisi Kiwira baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha Nne.Kituo cha Polisi Tukuyu mahali ambako Diwani wa Kata ya Kiwira Lawland Mwakalibule anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtoto wa shule ya Sekondari Kiwira.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa ambaye ni Diwani wa kata ya Kiwira anatuhumiwa kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha Nne shule ya Sekondari Kiwira.
Kamanda Diwani alisema kuwa wazazi wa binti huyo Rafael Frank(42) na mkewe Suzan Frank(38) waligundua kutoweka kwa mazizngira ya  kutatanisha kwa binti yao mwenye umri wa miaka 18 (jina linahifadhiwa)ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha Nne.
Alisema kuwa mara baada ya wazazi hao kutomwona binti yao chumbani walitoa taarifa kituo cha polisi cha Kiwira ambapo jitihada za kumsaka binti yao zilifanyika usiku kucha bila mafanikio ambapo majira ya saa tatu asubuhi alirejea nyumbani ndipo wazazi walipomuuliza alikokuwa na kusema kuwa alikuwa kwa mtuhumiwa ambaye ni Diwani wa kata ya Kiwira Laurent Mwakalibule(28).
Binti huyo alisema kuwa alilala nyumbani kwa mdogo wa mtuhumiwa hadi asubuhi baada ya kuwasiliana naye kwa njia simu.
§   


Post a Comment