Ads (728x90)

Baadhi ya wadau na viongozi wa soka la vijana chini ya miaka 15 wakiwa katika mkutano wa taarifa za kuanza kwa ligi hiyo

Add captionTIMU 6 za soka la vijana chini ya miaka 15(U-15) zinatarajia kuanza kutimua vumbi katika mchuano wa ligi hiyo unaozikutanisha timu kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
Akizungumzia ratiba ya mashindano hayo Katibu wa chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Mbeya(MREFA) Suleiman Haroub alisema kuwa michuano hiyo inazikutanisha timu sita kutoka mikoa ya Iringa,Njombe,Mbeya, Ruvuma, Rukwa na Katavi.
Haroub alisema michuano hiyo inayoanza leo na kumalizika Septemba 6 itazikutanisha timu katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza litazikutanisha timu za Katavi,Njombe na Rukwa, ilhali kundi la pili litazikutanisha timu za Ruvuma, Mbeya na Iringa.
Wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Cocacola kwanza imetoa seti sita za jezi na mipira miwili kwa kila timu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi seti za jezi kwa viongozi wa timu hizo, Meneja mauzo na masoko wa kampuni ya Cocacola kwanza kanda ya Mbeya Jayanti Vekarian alisema kuwa kampuni yake imejitolea kudhamini soka la vijana wa chini ya miaka 15 ili kuendeleza na kuibua vipaji vya soka nchini.
Vekaria alisema kuwa kampuni ya Cocacola kwanza iko mbioni kuwapeleka wachezaji nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo zaidi kwa nia ya kuendeleza na kukuza vipaji vya soka nchini.
Naye mjumbe wa kamati ya ya maendeleo ya soka la vijana wa (TFF) Daud Yasin alisema kuwa washindi wa kwanza na wa pili katika michezo hiyo wataenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya kukutana na washindi kutoka kanda zingine.

Post a Comment