Ads (728x90)

Mtungo katika bodaboda katika barabara nyembamba ambayo inakatiza katikati ya mto mrefu wenye mamba wakali

Hapa wakitafakari namna ya kufika kijijini ambako usafiri wake ni bodaboda kukatiza katika mto wenye mamba

Barabara nyembamba inayokatiza katika mto mkubwa wenye mamba, hapa jamaa roho juu juu

Jamaa wamemkumbatia mwendesha bodaboda kuvuka katika barabara nyembamba inayokatisha kwenye mto mkubwa, mwingine akiogopa kupita akiwa amesimama mwanzoni mwa njia nyembamba anaonekana kwa mbaali

Jamaa walipovuka wakajiona ni mashujaa ilhali walipoikuwa katikati ya mto nusura waloweshe sarawili zao

Huyu alishindwa uvumilivu akajikaza kiume na kupita kwenye kijinjia huku akitetemeka na kuvuka

Pamoja na woga wa wageni kupita katika njia hiyo, wenyeji walikuwa wakipita huku wakiwa na shehena ya mizigo kama wanavyoonekana wakazi hawa wa kijiji cha Ngana wakiwa wamebeba mihogo katika baiskeli


kumalizika kwa safari ilikuwa ni namna ya kutafakari kuupata msosi ghafla wakaivamia mihogo iliyokuwa ikikaangwa kwa mafuta ya mawese kutuliza njaa

Baada ya kuona njaa inauma sana ilibidi waombe msaada wa kisu ili kujisevia kukatakata kachumbari na kulumangia kwa mihogo

Ilikuwa ni taabu tupu mara baada ya kumaliza kula na kumaliza kazi iliyopwapeleka kijijini  ikawa ni wakati wa kutafuta usafiri wa kurejea mjini, usafiri nao sio wa kimjini mjini, ndani ya gari ni mminyano mtupu watu watano watano,  ukijifanya mjanja unabaki kijijini na hapo inakula kwako


Post a Comment