| Eneo hili kama linavyoonekana pichani linajitambulisha ni wapi, hapa ndipo panapozalishwa bidhaa za matunda kama vile Tomato Sauce na Chilli Sauce |
| Pamoja na kuzalishwa bidhaa hizo muhimu za chakula ambazo zinapendwa na walaji wengi nchini lakini mazingira yake yameanza kuwatia kero wapita njia kutokana na harufu kali inayotoka eneo hilo |
| Nje ya jengo hilo linalozalisha bidhaa hizo kuna ghuba linalovuja maji yenye uvundo kamalinavyoonekana pichani na hivyo kusababisha wapita njia kuziba pua |
| Pamoja na ghuba hilo kujaa takataka zinazotoa harufu katika kiwanda hicho, hakuna jitihada zozote zinazoonekana kufanywa ili kuondoa kero hiyo kwa wapita njia |
Post a Comment