Ads (728x90)

Watoto hawa wanaopaswa kuwa shuleni nyakati kama hizi, walikutwa na kamera yetu wakifanya kibarua cha kusommba mchanga katika eneo la Sinde Jijini Mbeya, pamoja na jitihada za serikali kupinga ajira kwa watoto bado jamii inaendelea kuwatumia watoto kwa ujira mdogo
Mkazi wa Chunya mkoani Mbeya akiwa amebeba pakacha lenye bidhaa mbalimbali akisafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, usafiri wa baiskeli wilayani Chunya ni moja ya nyenzo muhimu za usafirishaji zinazorahisisha ubebaji wa mizigo.

Baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo katika eneo la Kabwe jijini Mbeya wakiendesha biashara zao karibu na barabara bila kujali madhara yanayoweza kutokea kutokana na eneo hilo kupitiwa na magari kuelekea katika stendi ya daladala zinazofanya shughuli zake Jijini Mbeya.

Mtaro huu wa maji machafu uko kando ya Uwanja wa Mpira wa miguu wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya, uwanja huo kwa sasa unatumika kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu, mkoa wa Mbeya unawakilisha timu mbili za Mbeya City na Prison.Post a Comment