Ads (728x90)

Basi la timu ya Yanga ambalo limevunjwa kioo na kumjeruhi dereva wa basi hilo Maulid Kiula kama anavyoonekana pichani chini

Meneja wa Uwanja wa Sokoine Modestus Mwaruka akiwa na mayai matatu yaliyochorwa chorwa ambayo alidai kuwa ameyakuta katikati ya uwanja
Mashabiki wa timu ya Mbeya City wakiishangilia timu yao
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiishangilia timu yao katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya jioni hii
Kocha wa Timu ya Yanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mechi kati ya timu yake na Mbeya City timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo akionesha fedha taslimu sh. milioni mbili ambazo aliahidi kuizawadia timu ya Mbeya City iwapo ingeshinda mchezo huo, hata hivyo alitoa sh. milioni moja baada ya timu hiyo kutoka sare

Mchezaji wa timu ya Yanga aliyefungiwa mechi sita kwa kujisajili timu mbili akiwa ni miongoni mwa mashabiki waliohudhuria kuangalia mechi kati ya timu yake na Mbeya CityMpambano kati ya timu mbili za ligi kuu Yanga ya Dar es salaam na Mbeya City ya Mbeya umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.Mchezo huo ambao ulitawaliwa na shamrashamra na hoihoi uwanja mzima ulikuwa ni wa vuta nikuvute ambapo hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimetoka uwanjani suluhu bila ya kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitaka kupata bao la kuongoza, bahati iliwaangukia timua Mbeya City mnamo dakika ya 45 ambapo mchezaji Mwagane Yeya alitumia udhaifu wa walinzi wa timu ya Yanga na kufanikiwa kuipatia timu yake bao ambalo lilifungwa kwa kichwa na kumuacha golikipa wa timu ya Yanga Ali Mustafa Baltez akigaa gaa pembeni huku mpira ukiwa umetinga wavuni.
Mara baada ya bao hilo la Mbeya City Yanga ilianza kulishambulia lango la Mbeya City kwa kasi kubwa na kusababisha dakika ya 65 golikipa wa timu Mbeya City kuutema mpira ambapo mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete aliusukumia wavuni lakini goli hilo lilikataliwa na mwamuzi  Andrew Shamba.
Mnamo dakika ya 71 Yanga ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia mchezaji Didier Kavumbagu ambaye aliwatoka walinzi wa timu ya Mbeya City na kutumbukiza bao kimiani,hadi kipyenga kinapulizwa mabao yalikuwa sare ya 1-1.
Awali mchezo huo ulitawaliwa na vituko na vurugu za hapa na pale ambapo kabla ya mechi hiyo kuanza wakati wachezaji wa timu ya Yanga wanaingia uwanjani na Basi lao kundi la mashabiki wa timu ya Mbeya City walianza kuvurumisha mawe na chupa na kusababisha Basi hilo kuvunjwa kioo cha upande wa dereva Maulid Kiula na kumjeruhi mkono wake wa kulia.
Aidha kituko kingine kilichotokea kabla ya mchezo huo kuanza ni kukutwa mayai matatu yaliyochorwachorwa katikati ya uwanja ambapo Meneja wa uwanja huo Modestus Mwaruka aliyaondoa na kuyapeleka ofisini.
Post a Comment

  1. soka katika mazingira haya haliwezi kutupeleka mbali.Tujirekebishe

    ReplyDelete