Ads (728x90)

Wajumbe wa ALAT Katavi walipotembelea mradi wa ujenzi wa Bweni la wanafunzi Shule ya Sekondari Kabungu


Na Kibada Kibada –Katavi.
Wajumbe wa Jumuiya ya serikali za Mitaa tawi la Mkoa wa Katavi (ALAT) wameshauri serikali kuangalia utaratibu  mpya wa sheria za manunuzi kwa kuwa  matumizi ya wakandarasi inachelewesha kazi pamoja na kuchukua gharama kubwa  mno katika utekelzaji wa shughuli.
Ushauri  huo ulitolewa na wajumbe hao mara  baada ya  kutembelea miradi  mbalimbali ya ujenzi wa Maabara,Maktaba na Mabweni yanayojengwa katika Kata ya Kabungu kwenye shule za sekondari  kwa gharama ya Shilingi milioni 72  katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Wajumbe hao walikagua ujenzi wa Bweni na Maabara katika shule ya Sekondari Kabungu kazi iliyofanywa na mafundi wa eneo hilo bila kuwatumia Wakandarasi ambao awali alishindwa kukamilisha ujenzi kwa wakati.
Awali Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Estoming Chang’ah.aliwaeleza wajumbe hao kuwa kutokana na muda Halmashauri waliamua kuwatumia mafundi wa kawaida walioko kwenye eneo husika ili kukamilisha ujenzi wa maabara baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kukamilika kufuatia  mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kushindwa kukamilisha kandarasi hiyo kwa muda.
Chang’ah alieleza Halmashauri baada ya kupewa agizo na  Mkuu wa Mkoa kuwa maabara zote katika Mkoa zinatakiwa kukamilika ifikapo mei 30 mwaka huo walilazimika kutafuta fedha na kuwatumia mafundi walioko katika maeneo husika kwa kile kilichoelezwa kuwa iwapo wangetumika wakandarasi kazi isingeweza kukamilika.


Post a Comment