Ads (728x90)
TUJIKUMBUSHE      OCTOBA,2002
Na Rashid Mkwinda, Mbeya
JESHI la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili wakiwa na milipuko 675 aina ya  baruti na waya mbili wakiziingiza nchinini kupitia njia za panya katika mji mdogo wa Tunduma uliopo mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Said Mwema aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Muziki Michael(32) na Shungu Mponzi(23 raia wa Tanzania ambao walizifunika baruti hizo na vitenge zikiwa ndani ya sanduku.
Kamanda Mwema alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na Polisi waliokuwa Doria Septemba 29 mwaka huumajira ya saa 1:15 usiku wakiwa na baruti hizo ambapo baada ya kuhojiwa ilibainika kuwa hawakuwa na kibali cha kuingiza nchini.
Alisema ilibainika kuwa watuhumiwa hao waliingiza milipuko hiyo kwa nia ya kuwapelekea wavuvi na wachimba madini huko wilayani Chunya, Watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka wamepelekwa rumande baada ya kukosa dhamana.
Katika tukio jingine mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Chalangwa wilayani Chunya aliyefahamika kwa jina la Hans Chapa(70) amefariki dunia akiwa ndani ya nyumba baada ya nyumba yake kuteketea kwa moto.
Kamanda Mwema alisema kua tukio hilo lilitokea Octoba 10,2002 majira yab saa 1:00 usiku baada ya nyumba aliyokuwa akiishi marehemu kushika moto uliowashwa ndani kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma nyakati za usiku.
Kamanda Mwema amewaonya wananchi kuwa na tahadhari juu ya matumizi ya moto na kutoacha moto nyakati za usiku ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Post a Comment