Ads (728x90)


                                                                   
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenister Mhagama
Jenister Mhagama

Baadhi ya Wanafunzi wa shule moja  ya Sekondari Nchini.(Picha kwa hisani ya Mtandao)
                                                                                                        
Na Kibada Kibada –Katavi,
IMEEELZWA kuwa serikali bado haijaweka sera kwa wanafunzi wanaopata ujauzito mashuleni kurejea kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
Hayo yamebainika katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda hivi karibuni na Kaimu Ofisa Elimu wa Sekondari Stephen Masungwa akifafanua hoja iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima kutaka wanafunzi wanaopata ujauzito kurejea mashuleni.
‘’Hadi sasa hakauna sheria inayoruhusu wanafunzi waliopata ujauzito mashuleni kuendelea na masomo, Wizara bado haijaweka sera juu ya jambo hili,’’alisema Masungwa.
Alisema kuwa agizo la Mkuu wa Wilaya ni gumu utekelezaji wake hivyo utaratibu uliopo wa kubaki majumbani baada ya kupata ujauzito ndio unaoendelea.
Kwa upande wake Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mrisho Malaka  alieleza kuwa  ipo sheria  inayosema kuwa mwanafunzi anayeanza shule lazima amalize shule kwa mjibu wa sheria ya elimu ya mwaka 1978 pamoja na kanuni ya Elimu ya Mwaka 2003 pia sheria hiyo inasimamiwa na mabaraza ya Kata ambapo adhabu zinatolewa huko.
Awali katika Kikao hicho cha Baraza la Madiwani Diwani wa Viti Maalum Theodora Kisesa alielezea tatizo la kukithiri kwa utoro na mimba mashuleni kuwa linachangia kuzorotesha maendeleo ya elimu wilayani humo.
Alisema kuwa wanafunzi wengi wamekatisha masomo kutokana na kuwa wajawazito na wanafunzi hao hasa wale waliomaliza elimu ya msingi na kujiunga na sekondari wamejifungua watoto na wako majumbani hali ambayo inachangia kudorora kwa elimu kwa wanafunzi wa kike.
Naye Diwani wa Kata ya Kabungu Selemani Kasonso alieleza kuwa mbali ya mimba pia upo utoro wa reja reja ambao kwa wingi ambao umekithiri kwa kasi ilhali hakuna  hatua zozote za zinazochukuliwa na wazazi kuthibiti utoro huo pamoja na walimu kujitahidi kuwahimiza wazazi kujali elimu.
Diwani wa Kata ya Mpanda Ndogo Ahmed Mapengo alihoji utekelezaji wa agizo la Mkuu wa wilaya hiyo Mwamlima ya kutaka wanaokatiza masomo kwa kuolewa, kuoa au kupata ujauzito kurejea madarasani mara shule zitakapofunguliwa Mwezi Julai.



Post a Comment