Ads (728x90)

Golikipa wa Timu ya Kdege akichupa kuuokoa hatari kutoka kwa mchezaji wa Green City Castro Castro

Timu za Green City Vs Kadege FC kabla ya mpambano wa michuano ya Castle Lager Perfect 6 katika viwanja vya shule ya Msingi Mwenge Jijini Mbeya ikiwa ni michuano ya kumpata mshindi wa kuungana na timu za kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya kuwapata washindi watakaoiwakilisha Tanzania nchini Spain, katika mchezo huo Green City iliifunga Kadege 3-1.


Wachezaji wa timu ya Green City Issa Nelson na Castro Castro wakiwania mpira huku mchezaji wa Kadege FC akiwa amedondoka chini katika mchuano wa kuwania kwenda Spain, mchezo huo wa soka unahusisha wachezaji 6 kwa kila timu.

Patashika katika lango la Kadege, golikipa wa Kadege akiruka juu kuokoa hatari huku mpira ukitoka juu ya mwamba baada ya shuti ya mchezaji wa Green City Issa Nelson.

Post a Comment