Ads (728x90)

Mkurugenzi wa Binslum Company Mohamed Binslum akiangalia jezi zenye mwonekano mpya za  timu ya Mbeya City huku Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya akiangalia

Mkurugenzi wa Binslum Mohamed Binslum akisoma taarifa za mkataba wa udhamini baina ya kampuni yake na timu ya Mbeya City

Meneja wa Timu ya Mbeya City Emmanuel Kimbe akishikana mkono wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Binslum ya Jijini Dar es salaam ambao wameidhamini timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili wa sh. milioni 360

Baadhi ya wanahabari wakijadiliana wakati wa halfa fupi ya utiaji saini ya udhamini wa klabu ya Mbeya City leo asubuhi


Timu Meneja wa Mbeya City Emmanuel Kimbe
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt. Samwel Lazaro

Mkurugenzi wa kampuni ya Binslum, Mohamed Binslum


Add captionTIMU ya Mbeya City ambayo ilicheza Ligi Kuu msimu kwa mafanikio makubwa jana imepata udhamini mnono wa sh.milioni 360 kwa miaka miwili kutoka kampuni ya Binslum ya  Jijini Dar es salaam.
Mbeya City iliyojizolea sifa lukuki kwa mtindo wake wa kuzidindia timu zote zilizocheza ligi Kuu msimu uliopita imewashawishi wadhamini hao kuwekeza kwa timu hiyo kwa nia ya kuongeza chachu kwa timu za mikoani zinazocheza Ligi Kuu.
Akizungumza wakati wa utiani saini wa mkataba huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji leo asubuhi, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mohamed Binslum alisema udhamini wao umelenga kuleta changamoto na hamasa kwa timu za mikoani.
Binslum alisema kuwa wameamua kuwekeza kwa Timu ya Mbeya City kutokana na namna ambavyo timu hiyo imeonesha mtindo wa kipekee wa ushawishi kwa soka hapa nchini kinyume na ilivyozoeleka kwa timu kubwa za Yanga na Simba.
Alisema kuwa kampuni ya Binslum inaamini itanufaika kwa kutangaza bidhaa zake kupitia jezi za timu hiyo katika michezo yake kwa msimu wa mwaka 2015-16 na kuwa wamefikia makubaliano hayo na uongozi wa Mbeya City kutokana na mwitikio mkubwa wa wapenzi wa soka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Awali akizungumza katika hafla hiyo fupi ya utiaji saini mkataba na kampuni hiyo Meneja Mbeya City Emmanuel Kimbe alisema kuwa anaamini ufadhili huo utachangia kuiongezea uwezo timu hiyo katika ligi Kuu msimu ujao wa 2015 na 2016.
Alisema kuwa mkataba huo utachangia kuongeza kipato cha timu hiyo na kuiwezesha kujikimu kwa matatizo madogo madogo ambayo anaamini yatatatuliwa kwa ufadhili huo wa miaka miwili.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambaye ndiye mmiliki wa timu hiyo Dkt. Samwel Lazaro alisema kuwa ufadhili kwa timu za mikoani utachangia klabu nyingi zisizo na uwezo wa kifedha kushiriki ligi kwa ushindani katika ligi na kukua kwa soka la Tanzania.

Post a Comment