Ads (728x90)



Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ni mwenyeji wa Mpanda ambako wanafunzi wanakosa masomo kwa kukosa maji akizindua wiki ya Maji Mjini Dodoma


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa



Na Kibada wa Kibada -Katavi

WANAFUNZI wa shule ya Sekondari  Mpanda Ndogo iliyopo katika Halmashauri ya Mpanda wilayani Mpanda mkoani Katavi wamelazimika kusafiri umbali wa km 2 kufuata maji yam to kwa ajili ya matumizimbalimbali shuleni hapo.

Wakizungumzia hali hiyo hivi karibuni mbele ya Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso aliyefanya ziara shuleni hapo baadhi ya walimu wa shule hiyo walisemaa moja ya tatizo linaloikabili shule hiyo ni tatizo sugu la Maji safi na salama.

‘’Tunakabiliwa na tatizo la maji safi na salama, wanafunzi hulazimika kutembea zaidi ya kilomita mbili kufuata maji mtoni,’’alisema Rashid Msyete Mkuu wa shule hiyo.

Msyete alisema kuwa mbali na ukosefu wa maji shule hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa vitabu vya masomo ya sayansi ikiwa ni pamoja na tatizo la utoro kwa baadhi ya wanafunzi na kukosekana kwa mlezi wa wanafunzi wa kike wanaokaa Bweni. 
 
Alisema tatizo hilo la maji limewasababisha kuvunja baadhi ya vipindi kwa ajili ya kusaka maji na hivyo kusababisha kudorora kwa taaluma kwa wanafunzi hao kwa kuwa muda mrefu wanakuwa nje ya masomo wakisaka maji.

Kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo Walimu wa shule hiyo walimwomba Mbunge wao kusaidia kwa namna moja ama nyingine katika kulipatia ufumbuzi tatizo hilo sugu ambalo mbali na kusababisha kudorora kwa elimu linachngia utoro shuleni.

Kwa upande wake Mbunge Kakoso aliagiza Kamati ya Maendeleo ya Kata(KAMAKA) kuketi ya uongozi wa Halmashauri ya wilaya kuangalia uwezekano wa mfuko wa jimbo kusaidia katika uchimbaji wa kisima shuleni hapo kwa nia ya kuondoa kero hiyo.

Post a Comment