Ads (728x90)

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso akimkabidhi msaada wa vifaa vya umeme mmoja wa walimu wa Sekondari Karema kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wapate fursa ya kujisomea nyakati za usiku.

Mbunge wa Mpanda vijijini Moshi Kakoso mwenye fulana  ya pundamilia akiwa na viongozi na wa serikali na wazazi katika moja ya shule ya msingi Isengule   Kata ya Ikola akikagua madawati aliyowakabidhi walimu kama yanatumika kama ilivyokusudiwa

Mbunge wa Mpanda Vijijini Moshi Kakoso akikagua tanki la maji lilojengwa katika kijiji cha Ngomalusambo kwa ajili ya kuwasaidia wnanchi kuondokana na kero ya maji, wengine ni Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Paul Kahoya mwenye suti ambaye alimwakilisha Mkurugezi wa Halmashauri hiyo na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mpinduzi wa kata hiyo.


Na Kibada Kibada –Katavi.
Mbunge wa Mpanda Vijijini Moshi Selemani Kakoso  ametoa misaada ya mbalimbali ya kijamii katika kuinua elimu jimboni ikiwa ni pamoja na kugawa computer Mpakato ‘laptop’ kwa shule zote  za sekondari  zilizoko kwenye jimbo  lake.

Kakoso pia amesaidia  vitabu vya  masomo ya sekondari kwa shule za Sekondari Karema,Mpanda Ndogo Sekondari pamoja na kusaidia  madawati 600 kwa shule zote za msingi 50 katika jimbo hilo katika kukabiliana na changamoto za madawati zinazoikabili shule nyingi za sekondari katika mkoa wa Katavi.

Shule zilizonufaika na Kompyuta Mpakato ni pamoja na Shule ya wazazi ya Milala,Karema,Kabungu,Mpandandogo,Ilandamilumba,Mwese,Karema.Ikola,na Mishamo ambazo zimo katika jimbo lake mbali ya kutoa Kompyuta hizo pia alisaidia kuweka umeme wa jua kwa kutumia mfuko wa jimbo kwenye sekondari hizo na zahanati ili kuhakikisha masomo yanatolewa kwa nyakatio zote.

Pamoja na msaada huo amewagawia vijana jezi na mipira ili kuendeleza sekta ya michezo katika jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa vijana wa kike na kiume kuunda vikundi vya uzalishaji mali kwenye Mashina ya Wakereketwa na kuwawezesha mitaji kwa kila Shina kiasi cha shilingi 500,000 ili waweze kuanzisha miradi ya uzalishaji mali waweze kujitegemea.

Aidha Walimu wa kila shule kati ya 50 katika jimbo hilo amewawezesha kwa kuwapa mtaji wa shilling laki moja moja ili kuanzisha miradi ya uzalishaji kwenye shule zao ili kupunguza ukali wa maisha kutokana na walimu hao kutegemea mishahara pekee kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

Post a Comment