Ads (728x90)


Mkulima wa Pareto kutoka Igoma wilaya ya Mbeya William Mwakatobe akielezea tatizo la wakulima kukopwa maua ya pareto na kucheleweshewa malipo yao ya pili
Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Wadau wa Pareto Lawrence Tara akifafanua jambo katika kikao cha Wadau wa Pareto mjini Makambako Njombe
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Awariywa Nnko akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa Pareto Makambako

Mkurugenzi wa Bodi ya Pareto Ephraim Mhekwa akitoa ufafanuazi katika kikao cha Wadau wa Pareto kilichofanyika Makambako mkoani Njombe mwishoni mwa wiki.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Makete Mkoani Njombe imedai kuwa wanunuzi wa zao la Pareto wamekuwa wakikwepa ushuru kwa kununua zao hilo nyakati za usiku na kutoroka bila kulipa ushuru wa Halmashauri hiyo.
Hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Jison Mbalizi alipokuwa akichangia hoja kwenye kikao cha Wadau wa zao la Pareto kwenye Ukumbi wa Mid Town mjini Makambako mwishoni mwa wiki.
‘’Wanunuzi wanaingia Makete kinyemela nyakati za usiku na kununua pareto bila kulipa ushuru wa Halmashauri, huo ni wizi, tunaomba hatua zichukuliwe dhidi ya makampuni hayo,’’alisema Mbalizi.
Alisema kuwa Halmashauri haijalipwa ushuru kwa zaidi ya miezi sita huku kampuni zikiendelea kununua pareto ana kwamba kuna haja ya kudhibiti hali hiyo ambayo inapunguza mapato ya halmashauri yatokanayo na ushuru wa mazao.
Naye mkazi wa kijiji cha Tembela wilaya ya Mbeya William Mwakatobe alisema kuwa Bodi ya Pareto inapaswa kuangalia taratibu za wanunuzi ambao wanadhulumu haki za wakulima na kusema kuwa wakulima wamekuwa wakikopwa maua ya pareto na kugoma kulipa malipo ya pili.
Mwakatobe alisema kuwa kinachofanywa na kampuni ya ununuzi wa pareto ni kuchukua maua ya pareto kwa mkopo bila kulipa hivyo kusababisha wakulima wa zao hilo kutoona umuhimu wa kuendelea kulima zao hilo.
Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya PCT inayonunua Pareto wilayani Makete, Martin Oweka alisema kuwa kampuni yake itafanya jitihada za kulipa deni inalodaiwa na kwamba lipo tatizo kwa mawakala wao katika wilaya za  Makete,Mbeya Vijijini,Ileje, Mufindi na Kilolo.
Oweka alisema kuwa tatizo hilo(hakulifafanua) limesababisha kuwa na madeni kwa wakulima na kuwa hata hivyo watalipa madeni hayo baada ya mchanganuo muda mfupi ujao.
‘’Sio sera yetu kukopa, tunalipa kulingana na takwimu, tunapeleka fedha kila wiki inaonesha mawakala wetu ndio tatizo,’’alisema Oweka.
Kwa upande wake Mwanasheria kutoa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Shani Mayosa alisema kuwa kutolipa wakulima na kukwepa ushuru ni kosa na kwamba si jambo la busara kuendelea kutoa leseni ya biashara kwa wanunuzi ambao hawana manufaa kwa wakulima.
Aidha Mkurugenzi wa Bodi ya Pareto Ephraim Mhekwa alisema kuwa wanunuzi wanapaswa kuzingatia ubora wa zao hilo ili kukidhi viwango vya Kimataifa na kuwa serikali imeweka mkakati wa kuanza kuchoma maua ya pareto yasiyokidhi viwango ili kuwa na nidhamu ya kilimo bora cha Pareto nchini.

Post a Comment

  1. Hello dear mwombaji Mimi ni Mheshimiwa Stephen Brown kwa jina na i ni mmiliki wa Trust Fedha World Loan Company. Kwa heshima ya matendo yangu kubwa, mimi itabidi kama wewe kujua kwamba i kutoa kila aina ya mkopo unaweza milele kufikiria katika tu kiwango cha riba ya 3%. Harakisha sasa na kuomba kwa ajili ya mkopo wako haraka ili tuweze kupata mkopo wako mbio. Wasiliana nasi leo saa: trustfunds402@yahoo.com Omba kwa ajili ya mkopo wako leo na kupata hivyo kwa haraka kama unataka hivyo. * STEPHEN BROWN *

    ReplyDelete