Ads (728x90)





Unaweza kutafakari namna uishivyo wewe ukadhani kila mmoja anaishi kama unavyoishi wewe, ukipata fursa ya kujua namna ambavyo wanaishi wengine, utapata picha kuwa kumbe ipo haja ya kutafakari kwa kina aina ya maisha uishiyo kama yanakunufaisha wewe binafsi ama yanawanufaisha wengine.
Jawabu utakalo lipata japo si lazima unipe kwa wakati huu litakupa njia mbadala ya kuishi na jamaa zako kulingana na namna ambavyo wewe Mwenyezi Mungu amekujaalia uishi, Ni vyema ukajitazama mara mbili, na ukatafakari kwa kina aina hiyo ya maisha uliyonayo kama ni kweli yanastahili kuwa hivyo, ukilinganisha na maisha ya wengine waliopo katika eneo hilo hilo uishilo wewe.
Umejaaliwa kuwa na akili timamu za kutafakari aina ya maisha ambayo yanakustahili wewe kulingana na rasilimali zinazokuzunguka, Jee wewe ni wa aina gani ya maisha, unapata riziki yako kwa njia ipi, si lazima unipe jibu hapa, bali wapo wanaopata riziki kwa kufanya kazi za sulubu, na wapo wanaopata riziki kwa kukesha usiku kucha kama mbwa kuwalinda mabwana wakubwa.
 Pi wapo wanaopata riziki kwa kumwaga zege na mikono yao kubabuka kutokana na kazi hizo za sulubu, kadhalika wapo wanaopata riziki yao wakiwa wamekaa maofisini huku wakichezesha kalamu zao na kubadilisha tarakimu 30 na kuongeza tarakimu 300000000.... ili mradi kila mtu huelezwa kuwa hula kulingana na urefu wa kamba kama alivyo mbuzi.
Falsafa hii ya maisha ndiyo inayoweka tabakla baina ya mmoja na mwingine, aliyenacho na asiye nacho, Tajiri na Fukara. wote wanavuta Oksijeni na wanahitaji kuishi...naomba niishie hapa kwa kuwa kila ninapoendelea kuandika najihisi hasira dhidi ya wale wanaodhulumu haki za wanyonge na kujinufaisha matumbo yao na kusababisha mamilioni ya Watanzania wakibaki kuwa tegemezi katika maisha yao yoote!!!!!

Post a Comment