Ads (728x90)

Abubakari Muharram(13) mshindi wa kuhifadhi na kusoma Koran Tukufu Juzuu 10
Mmoja wa wadhamini wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Koran Jijini Mbeya Khalfan Masoud akimpongeza mshindi na msomaji wa koran aliyehifadhi Juzuu 10 Abubakar Muharram katika mashindano yaliyofanyika leo Jijini Mbeya katika msikiti mkuu uliopo BARABARA ya 8.
Mgeni rasmi katika mashindano ya kuhifadhi na kusoma Koran Adam Safari akimkabidhi zawadi msomaji wa Koran  Mtoto Mariam  Nzebele(5) aliyeshika nafasi ya 3 kusoma na  kuhifadhi Juzuu 1 kwenye mashindano ya usomaji wa Koran leo mchana.
Majaji wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Koran wakifuatilia kwa makini namna ambavyo vijana wakichuana kusoma na kuhifadhi Koran katika  msikiti wa Barabara ya 8 Sokomatola Jijini Mbeya.
Muongozaji wa mahindano ya Kusoma na Kuhifadhi Koran Ibrahim Bombo akimuongoza mshindi wa mashindano hayo aliyehifadhi Koran Juzuu 10 Abubakar Muharram kwenye mashindano yaliyofanyika leo mchana kwenye msikiti wa Barabara ya 8 Sokomatola Jijini Mbeya, Vijana 58 walishiriki mashindano hayo.
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Koran
Mshiriki wa kusoma na kuhifadhi Koran Tukufu Habiba Jafar akishiriki kusoma na kuhifadhi Juzuu 3 katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Koran Jijini Mbeya leo mchana
Sheikh mkuu wa mkoa wa Mbeya(BAKWATA) Mohamed Mwansasu akitoa nasaha wakati wa mashindano ya kusoma na Kuhifadhi Koran Tukufu leo mchana

Post a Comment