Ads (728x90)



 ANSWAR SUNNA WAWAPINGA  BOKO HARAM, AL-SHABABI
Ustadhi Ibrahimu Mkate akizungumza katika Ibada ya Swala ya Idd El Fitri kwenye Viwanja vya Kiwanja Ngoma Sokomatola Jijini Mbeya leo asubuhi.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa katika Ibada ya Swala ya Idd leo asubuhi.

Ustadhi Ibrahim Mkate akisisitiza jambo wakati wa ibada ya swala ya Id el Fitri leo asubuhi.
Waumini katika Ibada ya Swala ya Idd el Fitri Jijini Mbeya leo asubuhi. 

JUMUIYA ya waislamu wa Answar Sunna mkoani Mbeya wamesema kitendo cha mauaji na utekaji nyara kinachofanywa na makundi ya Boko Haram na Alqaida ni uovu unaopaswa kupingwa na waislamu kote duniani kwa kuwa si mafundisho ya dini hiyo.
Akizungumza wakati wa ibada ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani jijini Mbeya Kiongozi wa Kiislamu ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha King Saud kilichopo Riyadhi  nchini Saudi Arabia, Ustadh Ibrahimu Mkate alisema watu hao wanapaswa kuuawa kutokana na kupingana na mafundisho ya Uislamu.
Alisema kinachofanywa na watu hao kinapingana na dini ya Kiislamu hivyo waislamu wanapaswa kuungana kupinga vitendo hivyo ili kuunusuru Uislamu na waislamu duniani.
 ‘’Hii si mila ya dini ya Kiislamu inayohubiri amani na upendo, hawa wanaowaua watu wasio na hatia, mafundisho haya wanayatoa wapi,wanavaa mabomu na kujilipua na kuwaua watu wasio na hatia, akina mama, wazee na watoto, wao ndio wanaopaswa kuuliwa kwa kuudhalilisha Uislamu,’’alisema Ustadh Mkate.
Aliwakana watu hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakijivika jina la Kiislamu na kufanya mambo yanayoshabihiana na dini ya kiislamu kwa kuwaita kuwa ni makafiri ambao wanaupinga Uislamu.
 ‘’Hawa ni maadui wa Uislamu, uislamu unafundisha Amani na Upendo, wanatuchafua waislamu, sisi hatufundishi kuuana bila hatia,  zipo sheria zinazotanabahisha nani wa kuuliwa kwa wakati gani na kwa sababu gani,
Aliendelea kusema kuwa  makundi ya Alshabab, Boko haram, Alqaida  ni makundi yasiyofaa katika Uislamu na kwamba kitendo chao cha kuvaa mabomu na kujilipua ni ukafiri ambao hauendani na mafundisho ya Uislamu.
Alibainisha kwa kusema kuwa hiyo si Jihadi kama inavyotafsiriwa bali ni ukatili na unyama unaofanywa na maadui wa Uislamu ili kuuchafua na kuwa mafundisho ya Muhammad (SAW) kwa waislamu yalikuwa ni kuingia vitani kupigania dini yao kwa haki dhidi ya wale wanaowapinga na kuwaua bila haki na sio kuua wasiokuwa na hatia.
‘’Hakuna Sheria ya kujilipua mabomu kwa waislamu, hiyo sio Jihadi iliyosemwa, huo ni Ukafiri na wanaofanya hivyo ni Makafiri sio waislamu,’’ alisema.

Post a Comment