Ads (728x90)

Akina mama wa Kiislamu wakishiriki katika Mchezo wa kuvuta kamba kwenye Tamasha la Eid El fitri kukamilisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jana jioni, michezo mbalimbali ilifanyika ikiwahusisha akina mama, akina baba na watoto.

Akina baba nao hawakuwa nyuma katika michezo nao walishiriki kwenye mchezo wa kuvuta kamba ili kupimana nguvu baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan
Waislamu pia walijitokeza katika mashindano ya mbio za baiskeli ili kukamilisha burudani ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan Jijini Mbeya.

 Huku wengine wakishindana katika kukimbia na magunia wengine walishiriki katika mchezo wa kufukuza Kuku, ili mradi ilikuwa ni burudani ya aina yake kwa Waislamu na baadhi ya wakazi wa Jiji la Mbeya ambao walihudhuria kushuhudia tamasha hilo la aina yake ndani ya Uwanja wa Sokoine.
Baadhi ya akina mama wa Kiislamu wakijiandaa kwa mchezo wakati wa Tamasha la Eid El Fitri katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya jana alasiri.
Mbali na michezo mingine iliyofanyika, kulikuwa na mchezo mwingine wa kuvutia wa mashindano ya Kukuna Nazi kwa akina baba na akina mama
  

Aidha Tamasha hilo la Eid El fitri lilihitimishwa kwa mechi ya burudani kati ya Maimamu na timu ya Mbeya City kikosi cha pili ambapo Mbeya City waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Benchi la Ufundi la timu ya Maimamu
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia michezo mbalimbali ya Tamasha la Eid El Fitri kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine


Golikipa wa timu ya Maimamu Maisara Mwakibinga akiokoa shuti kutoka kwa mchezaji wa MBEYA CITY kwenye mechi ya kirafiki kati ya timu hizo kuadhimisha kukamilika kwa mfumgo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan

Wachezaji wa Mbeya City wakipata mawaidha baada ya kumalizika kwa mechi kati yao na timu ya Maimamu
Awali wakati wa adhuhuri baadhi ya waumini wa dini hiyo walipata fursa ya kualikwa kwenye chakula cha mchana nyumbani kwa mmoja wa waumini hao Amour Sumry
Walikula chakula na vinywaji na kushiba kabla ya kuingia kwenye tamasha la Eid
Vyakula aina mbalimbali viligaiwa kwa Mashekhe ambao walikula na hatimaye kusaza!!! nadhani hii ilitokana na matumbo yao kutozoea kula mchana kwa takribani mwezi mzima wa funga ya Ramadhan
 

Post a Comment