Ads (728x90)


Na Kibada Kibada -Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe amewataka vijana kote mkoani Katavi kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo mkoani humo ili kujikomboa kuondokana na umasikini kwa kufanya kazi kwa bidii na kutumia fursa zilizopo mkoani humo.
Dkt Rutengwe ametoa rai hiyo wakati akikabidhi msaada wa Mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa na shirika la nyumba la Taifa Mkoani Katavi kwa vikundi vya Vijana waliojiunga Pamoja kuanzisha miradi ya maendeleo itakayowaondolea umasikini.
Mbali ya kutoa wito kwa vijana kutumia fursa hizo pia amewaasa wazazi wote mkoani huo kuzingatia elimu kwa vijana wao kwa kuwa elimu pekee ndiyo itakuwa mkombozi wa maisha ya mwanadamu bila elimu hakuna maendeleo.
Akawahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao shule ili waweze kupata elimu  na wale ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari wawapeleke kwenye vyuo vya ufundi stadi Veta wapate elimu ya ufundi ambayo itawasidia katika maisha ,kwa kuwa watakuwa na ujuzi utakao wawezesha kujitegemea kwa kufanya kazi mbalimbali katika jamii kama ufundi wa ujenzi na ufundi mwingine
Amewaasa vijana watumie nafasi hiyo waliyopata ya kupewa misaada ya mashine za kufyatua tofali ili iwe chachu ya maendeleo kwao na kiw kichocheo kwao kujileta maendeleo na vijana wengine waige kutoka kwao.
Awali Meneja wa SHIRIKA LA nyumba Mkoani Katavi na Rukwa Nehemia Msigwa alieleza kuwa Shirika la nyumba Mkoani Katavi limetoa misaada ya mashine za kufyatulia Tofali kwa vikundi vya vijana kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Katavi ili ziweze kuwasaidia vijana kujikwamua na umasikini kwa kuanzisha miradi ya ufyatuaji tofali.
 Msigwa alieleza kuwa shirika lake limeamua kutoa msaada huo ili kuwasaidia Vijana kujianzishaia miradi yao ili waweze kujiali kupitia kwenye miradi ya ufyatua tofali kwa kutumia mashine hizo ambazo ni imara na bora na matoafali yanayotokana mashine hizo ni bora na imara hivyo wataweza kuondokana na umasikini .
Msigwa ameleza kuwa shirika  la nyumba limebuni mpango wa kuwasaidia vijana kujiajili  kwa kutumia mpango wa kuwasaidia vijana mashine ya kufyatu matofali ili kuwaondolea  umasikini na limetoa mashine nne kwa kila Halmashauri za wilaya ziweze kuwasaidia vijana kuondokana na umasikini na Halmashauri kupitia Idara za Maendeleo ya Jamii Kitengo cha Vijana watasimamie miradi hiyo.
Amezitaja Halmashauri  hizo kuwa ni Mpanda Mji ambayo imekabidhiwa mashine nne na mbili wamenunue wenyewe kuwasaidia Vijana ,Halmashauri ya Mpanda, Halmashauri ya Mlele na Nsimbo
Mbali ya kutoa msaada wa mashine za kufyatua tofali kwa makundi ya vijana hao  walijiunga pamoja katika vikundi vya uzalishaji mali ili kuondokana na umasikini  pia  Shirika hilo limetoa fursa kwa vijana wenye utalaamu katika fani ya uselemara mkoani humo kujitokeza kufanya kazi kwenye shirika hilo mkoani humo ili waweze kujipatia kipato na kuondokana na umasikini.
Fursa iliyotolewa ni kwa vijana 20 wenye fani hizo na wengine kumi wenye fani ya ujenzi kufanya kazi katika shirika hilo mkoani hapo kwa watoto walimaliza elimu ya ufundi kupitia kwenye chuo cha ufundi stadi Veta Mpanda waweze kuaidia katika shughuli za ujenzi unaoendelea sehemu mbalimbali Mkoani humo.
Meneja huyo wa shirika la nyumba ametoa fursa hiyo kufuatia kuwepo kwa vijana wengi mitaani wakilalamika kuwa hakuna ajira wakati ajira zipo lakini hawazitumie Vijana hao kwa kile wanachodhani ajira ni maofisini tushirika la nyumba limekuja kuwawezesha vijana kujikomboa kuondokana na umasikini Mkoani humo.

Post a Comment