Ads (728x90)
















Sina Baba wala Mama, naishi na bibi yangu mzaa mama simjui baba yangu, mama yangu alifariki, sisomi shule, sina madaftari wala nguo za shule,nachunga ng’ombe wa jirani yetu, bibi yangu ni mkulima, tunapata chakula kwa kubangaiza, siku nyingine tunalala na njaa, bibi yangu ni mzee sana.
Ni kauli ya mtoto huyu(aliyejitambulisha kwangu jina lake)anayefikia umri wa miaka 12 mkazi wa kijiji cha wavuvi na wafugaji  (katika eneo hili nililotembelea)ambaye kwa kawaida alipaswa kuwa  shuleni akipata elimu.
Familia nyingi za maeneo ya vijijini zimekuwa katika kadhia za aina hii, maisha ya sulubu ndiyo waliyoyazoea, wameyakubali na kuyafanya kuwa ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Ni nadra kwa mtu wa kawaida kuyazoea maisha ya aina hii lakini ipo jamii ambayo imelazimika kuyakubali na kuyapokea maisha haya na kuyafanya kuwa ni sehemu ya maisha yao ya kawaida.
Ni vigumu kuizoea hali hii lakini haya ndiyo maisha ambayo jamii hii imeyazoea na kuyakubali aghalabu familia nyingi za mjini huishi maisha yenye nafuu ingawa pia huikumbana na dharuba za kila siku za kuishi chini ya dola moja, ni tabaka la watu wa kawaida, nao wameyazoea na kuyakubali maisha ya aina hii.
Unaweza kuyakubali au kuyakataa maisha ya iana haya lakini mazingira halisi ya kipato yanakushawishi uyakubali na uishi katika hali hiyo kwa kadri ambavyo Mungu amekujaalia.
Kilio cha jamii hii kinapaswa kuelekezwa wapi? Katika jamii yenyewe au kwa washika dhamana kwenye mhimili mkuu, walioshika mpini wakawapa makali walalahoi ili wagombanie kukatwa mikono yao.

Post a Comment