Ads (728x90)


Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini wakati wa kilele cha Jubilei ya miaka 75 ya kanisa la TAG
Rais Kikwete akisalimiana na viongozi wa dini mara baada ya kwuasili katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kwenye kilele cha Jubilei ya miaka 75 ya kanisa la TAG

Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa mkoa wa Mbeya wakifuatilia maadhimisho ya kilele cha Jubilei ya miaka 75 ya kanisa la TAG

Rais Jakaya Kikwete akifuatilia kwa makini sherehe za miaka 75 ya kanisa la TAG katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jana(kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.

Baadhi ya Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakichukua matukio wakati wa kilele cha Jubilei ya miaka 75 ya kanisa la TAG katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

RAIS Jakaya Kikwete amevunja ukimya juu ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba mpya na kuomba usadizi kwa viongozi wa dini kusaidia kuombea Umoja ya Katiba ya Wananchi (UKAWA)kurejea katika mjadala a Bunge la Katiba ili hatimaye ipatikane katiba itakayokidhi matakwa ya Watanzania.
Akizungumza katika kilele cha Jubilei ya miaka 75 ya Kanisa la Tanzania Asembless Of God kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jana Rais Kikwete alionesha hofu yake ya kutokamilika mchakato wa kuundwa kwa Katiba hiyo iwapo UKAWA hawatarejea bungeni.
‘’Mjadala wa katiba ulianza vizuri walikubaliana kulingana na kanuni zao kuunda kamati 12, mjadala wa sura ya ya 1 na 2 ulichukua siku 19 badala ya siku 14 April 10 bunge lilikutana, April 13 taarifa  zote ziliwasilishwa, April 16 wajumbe wa CUF, CHADEMA na NCCR Mageuzi walitoka nje,’’alisema na kuongeza.
‘’Tena hawa ndugu zetu walitoka nje bila kuweka masharti ya kurejea kwamba kikifanyika hiki au kile watalegeza masharti yao, hawakutoa masharti ya kurudi, sisi matumaini yetu wote warudi ili wafanye maamuzi kwa pamoja,’’alisema Rais Kikwete.
Alisisitiza kuwa swala la kurudi ama kutorudi bungeni haliwatatizi viongozi wa dini pekee bali hata yeye binafsi na kwamba kuna haja ya viongozi wa dini kutumia nafasi yao kuwaombe wanaosababisha mgongano katika jamii ya Watanzania.
‘’Kama kuna mapepo ya kuombea, TAG mtuombee hili pepo la kutoelewana liondoke, wameanza mchakato kamati zote 12 zimekamilika kwenye mjadala wa jumla  mapepo yakaingia, huyu kamsema huyu na Yule kamsema mwingine, kama kuna mapepo waheshimwa hawa waombewe warudi wasafiane nia,’’aliendelea kusihi Rais Kikwete.
Hata hivyo Rais Kikwete alisema kuwa ameanza kupata matumaini baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mstaafu Francis Mutungi amefanya jitihada za kuwakutanisha viongozi wa vyama vikuu vinne vya siasa ambao wanaendelea mjadala juu ya hatima ya katiba.
‘’Batati nzuri wawakilishi wa CCM,CUF,CHADEMA na NCCR Mageuzi wanakutana, watokaje hapa ili waende mbele, nawapongeza viongozi wa vyama hivi, pia natoa pongezi maalum kwa Msajili wa vyama Jaji Mutungi, naamini hivi vyama vikubwa vinne vikikubaliana mambo yataenda.’’alisema.
Aidha aliwasihi wananchi kuwaachia nafasi viongozi hawa waendelee na mjadala wao bila kuingiziwa maneno mengine ambayo yatawakatisha tamaa bali wanatakiwa kupewa moyo.
‘’Watanzania wenzangu hebu tuwape nafasi hawa wajadili, kwa utulivu, tusiwachanganye,zaidi tunapaswa kuwaombea, miluzi mingi inampoteza mbwa usasi, unajua mbwa akipigiwa miluzi wakati wa kuwinda hawezi kwenda atasimama,’’alisema.
Rais Kikwete alishangazwa na baadhi ya watu ambao wanafanya kazi ya kupoteza umma kila jambo jema linapofanyika na kuonya kuwa iwapo kuna watu  wamechukua zabuni ya kuwalipa wanaoendeleza tabia hiyo ili serikali ifidie gharama za vitendo vyao.
‘’Wengine kazi yao ni kuongopa tu sijui tenda hii wanalipwa na nani kusema uongo, sisi serikali tutamlipa ili aache tenda hii ya kuvuruga watu, kazi yao ni kuvuruga watu wasielewane, hivi hili linatoka wapi, mwisho wa siku mtapandikiziana chuki na kuuana bure,’’alionya.
Awali akizungumza katika maadhimisho hayo Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Asembless Of God (TAG) Dkt.Barnabas Mtokambali aliwaomba wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambao wamesusia vikao vya Bunge hilo kurejea katika majadiliano ili iweze kupatikana katiba mpya itakayotoa mustakabali wa nchi yetu.
Alisema viongozi wa dini wamekuwa mstari wa mbele kuombea amani ya nchi na kuwa vitendo vya wajumbe wa Bunge la Katiba kususia vikao vya bunge hilo vinawakatisha tamaa wananchi na hivyo kukosa imani ya kuwa na Katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi wote.

Post a Comment