Ads (728x90)



Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Hawa Ghasia
Hawa Ghasia Waziri TAMISEMI
Na Kibada Kibada, Mlele
Halmashauri ya Nsimbo wilayani mlele mkoani katavi imefanikiwa kukusanyajumla ya shilingi milioni 753.04 na kuvuka lengo kwa asilimia 5.6 ya lengo lililowekwa la kukusanya jumla ya shilingi milioni 713,328.000.kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.
Hayo yamelezwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Rashid Neneka wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 kwenye kikao cha mkutano mkuu wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.
Neneka ameeleza kuwa  katika kikao maalum cha madiwani cha kupitisha bajeti kwa halmashauri hiyo ilipitisha kiasi cha shilingi bilioni 17,596,313,000 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.
baada ya kupata ukomo wa bajeti kutoka hazinaTAMISEMI makisio ya bajeti yamepungua kwa asilimia 22   hadi kufikia shilingi bilioni 13,682,949,500  kutoka vyanzo mbalmbali vya mapato
Neneka amevitaja vyanzo hivyo kuwa mapato ya ndani fidia ya vyanzo vilivyofutwa, miradi ya maendeleo.fedha za ndani fedha za wafadhili pamoja na vyanzo vingine.
Akizungumzia miradi ya maendeleo ameelezakatika kipindi cha robo ya pili yatu na yanne katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 idara ya mipango imepeleka kiasi cha fedha milioni 342 kwa ajili ya kutekeleza miradi  ya maendeleo kati ya fedha hizo milioni 282 zilielekezwa kwa sekta ya Elimu ya Msingi na shilingi milioni 60 zilielekezwa kwenye ujenzi sekta ya Elimu ya Sekondari.
Aidha ameeleza kuwa idara ya mipango ilisimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo madiwani walipita kuikagua katika ziara zao za kuhimiza  Miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 .
Miradi hiyo iko katika sekta ya Elimu, Afya,Maji,Utawala ,Barabara na Umwagiliaji,miradi ambayo imetekelezwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa maaendeleo 2013/2014.

Post a Comment