Ads (728x90)


 


TAFCA MBEYA
CHAMA cha Makocha mkoani Mbeya (TAFCA)kimepata uomgozi mpya kwa kuwachangua Katibu Mkuu wa chama hicho na viongozi wengine wanne kwa nia ya kuziba nafasi zilizoachwa wazi kwa takribani miezi nane.
Viongozi waliochaguliwa ni Katibu Mkuu wa chama hicho Joseph Singundali, Katibu Msaidizi Antony Mwamlima na wajumbe wawili  kamati ya Utendaji wa TAFCA Paul Msyaliha na Oscar Mboma.
Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Katibu wa chama cha mpira mkoa wa Mbeya Suleiman Haroub,ulifanyika jana katika Ofisi za Chama Cha Mpira wa Miguu mkoani Mbeya(MREFA) ambazo zipo katika Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine. 
Katika uchaguzi huo nafasi ya Katibu Mkuu iligombewa na wanachama wawili ambao ni Singundali na Emmanuel Mgalla ambaye alikaimu nafasi hiyo kwa miezi nane.
Nafasi hiyo ya Katibu Mkuu iliachwa wazi na Thomas Kasombwe ambaye amehamishwa kikazi nje ya mkoa wa Mbeya ilhali nafasi ya Katibu Msaidizi iliyochukuliwa na  Mwamlima ilikuwa wazi tangu uchaguzi mkuu uliopita.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kwa viongozi hao msimamizi wa uchaguzi Haroub alisema kuwa ana imani viongozi hao watasimamia vyema maadili ya kazi zao bila kuibua migogoro katika mchezo wa soka.
Alisema kuwa makocha ndiyo dira ya wachezaji na kuwa wachezaji wamekuwa wanaiga kila kinachofanywa na makocha hivyo iwapo kocha atakosa maadili na wachezaji pia wataiga tabia hiyo.
‘’Muwe mfano kwa wachezaji wenu mnaowafundisha, mkikosa maadili ndio mwanzo wa kuwaandaa vijana wenye vurugu na fujo katika mchezo wa mpira,’’alisema.
Pia alisema kuwa makocha hawapaswi kusubiri timu za kufundisha bali wao wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kusaka timu za mitaani ili kuibua vipaji vya vijana ambao ndio wachezaji wa baadaye.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Makocha Juma Mwambusi alisema kuwa dira ya michezo kwa wachezaji inatokana na makocha bora wenye uwezo na kwamba ni muhimu kwa makocha kuwaandaa wachezaji vijana ili kupata wachezaji bora.
 Akizungumza mara baada ya kushika nafasi ya Ukatibu Mkuu, Singundali alisema kuwa katika uongozi wake atahakikisha maadili ya walimu wa michezo yanasimamiwa vizuri ili kujenga nidhamu ya soka mkoani Mbeya.










Post a Comment