Ads (728x90)

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas KANDORO akitoa baraka za safari kwa wanahabari ofisini kwake leo asubuhi juu ya ziara yao ya kimafunzo katika nchi za MALAWI na ZAMBIA katikati ya mwezi Agosti
RC KANDORO akisikiliza kwa makini azma ya safari ya kimafunzo ya wanahabari nchini MALAWI na ZAMBIA


Baadhi ya wanahabari waliofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa leo saa moja asubuhi
Mmoja wanahabari Felix MWAKYEMBE akielezea mpango mkakati wa wanahabari juu ya azma yao ya kutembelea nchini Malawi na Zambia katikati ya AGOSTI.

Mkuu wa Mkoa Abbas KANDORO akifuatilia kwa makini maelezo ya wanahabari juu ya ziara yao katika nchi za MALAWI na ZAMBIA.

 

Wanahabari wakipewa Usia na Mkuu wa MKOA juu ya safari yao nchi za MALAWI na ZAMBIA
''Safari yenu, mna-cross Border zingatieni maadili ya taaluma yenu huko nchini kwa watu, hata hivyo mnapaswa kuwa Borden to Horizontals''
 

Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Ulimboka MWAKILILI akiagana na Mkuu wa Mkoa ambaye aliwatakia maandalizi mema ya safari yao.Ziara hiyo fupi kwa wanahabari iliwafikisha hadi kwenye ofisi ya Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Mbeya, Asumsio ACHACHA kama inavyoonekana pichani chini;
   


Ofisa UHAMIAJI mkoa wa MBEYA Asumsio ACHACHA akijitambulisha mbele ya wanahabari waliofika ofisini kwake leo asubuhi kwa lengo la kujitambulisha na kuelezea nia yao ya safari ya nchini MALAWI na ZAMBIA
Baada ya maelezo mafupi ACHACHA aliahidi kushirikiana na wanahabari kwa hali na mali na kuwataka wanahabari wasio na HATI za kudumu za usafiri(PASSPORT) watumie vyema ofisi yake ili waweze kukamilisha zoezi hilo mapema kabla ya safari
   
Mmoja wa wanahabari Christopher NYENYEMBE akiagana na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa baada ya kumaliza mazungumzo na kuwatakia maandalizi mema ya safari
Awali kabla ya kuingia ofisini kwa mkuu wa mkoa, wanahabari walifika ofisi ya Msaidizi wa MKUU wa mkoa  MASAYA na kuzungumza naye machache juu ya safari yao.
Katibu wa Mkuu wa mkoa MASAYA akiwasikiliza wanahabari kabla ya kukukatana Mkuu wa Mkoa.
 



MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa Asumsio Achacha wamewataka waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya ambao wanajiandaa na safari  ya nchini Malawi na Zambia kuwa wawakilishi na mabalozi wazuri katika kuutangaza mkoa wa Mbeya na Tanzania kwa ujumla.
Kandoro na Achacha walizungumza na wanahabari hao kwa nyakati tofauti leo asubuhi walipotembelewa ofisini kwao kwa nia ya kuelezea azma ya safari yao katika nchi za Malawi na Zambia katikati ya Mwezi Agosti.
Ziara hiyo ya wanahabari imeandaliwa na baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya ambao hujihusisha na habari mbalimbali za kijamii ikiwemo masuala ya utafiti juu ya mahusiano baina ya jamii ya ndani na nchi jirani.
Akizungumza na wanahabari hao baada ya kupewa taarifa za safari hiyo Mkuu wa Mkoa Kandoro alisema kuwa suala la mahusiano baina ya nchi na nchi ni jambo linalopaswa kuwekewa kipaumbele hususani katika mgogopro unaoripotiwa juu ya Tanzania na Malawi.
Alisema kwa kutumia fursa ya ziara ya wanahabari nchini humo itasaidia kuondoa fikra zilizopo kwamba kuna ugomvi baina ya nchi mbili hizi na kuwa mbali na ziara hiyo ya kimafunzo wanahabari wanatakiwa kuenda mbali zaidi ili kupata mengi ambayo yataendelea kuitangaza Tanzania na nchi jirani ya Malawi.
‘’Tumieni ziara yenu, kujifunza pia angalieni mengine yenye manufaa katika kuitangaza Tanzania, ‘’Borden to Horizon’’ hii itasaidia hata nchi jirani na Malawi kujua nini kilichopo Tanzania na kuwavutia,’’alisema.
Pia aliwataka wanahabari kutumia nafasi hiyo kutangaza fursa na vivutio vilivyopo nchini kwa nia ya kuwavutia wageni kutoka nchi hizo kutembelea nchini mwetu ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo katika kipindi cha mpito kwa mgogoro unaoelezewa kuwepo kuhusu mpaka wa nchi hizo.
Kwa upande wake Ofisa Uhamiaji wa Mkoa, Achacha alisema kuwa fursa ya wanahabari kutembelea nchi jirani za Malawi na Zambia zitaibua upya mahusiano baina ya nchi hizo na kuwa kwa kutumia kalamu za waandishi wa nchi zote mbili taarifa zitakazotolewa zitakuwa chanya.
‘’Mengi yanayoripotiwa ni Hasi, katika ziara yenu na wenyeji wenu wa  huko tutapata taarifa chanya, tumieni fursa hiyo kuelezea hali halisi ya mahusiano baina ya nchi zetu, nchi yetu haina Vita na Malawi,’’alisema Achacha.
Awali akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa Mwenyekiti wa kamati ya safari ya wanahabari hao, Ulimboka Mwakilili alisema kuwa azma ya safari hiyo ni ziara ya kimafunzo iliyolenga kujenga mahusiano baina ya nchi hizo kupitia wanahabari wa Tanzania na Malawi ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa na vivutio vilivyopo nchini.
Takribani wanahabari 25 wanatarajia kuanza safari yao ndefu kuelekea nchini Malawi na kutokea nchini Zambia na kurejea nchini katikati ya Mwezi Agosti.

Post a Comment